BILIONI 235 KUJENGA DARAJA LA JANGWANI DAR ES SALAAM
Moja ya Mambo makubwa yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ni kuendeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo iliyokuwa katika Mipango sambamba na kubuni Miradi mipya.
Mradi wa Uendelezaji Bonde la Mto Msimbazi ni mojawapo ya Mradi muhimu kwa Jiji la DSM hasa katika kupunguza na kuondoa kabisa adha ya Mafuriko inayolitesa Jiji hilo nyakati za Mvua.
Waziri wa Tamisemi, Mhe Ummy Mwalimu leo ameongoza kikao maalumu kati ya Tamisemi, Uongozi wa Mkoa wa DSM, TARURA na wataalamu wa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam (DMDP) kuzungumzia hatua zinazoendelea katika Mradi huo .
Kwa mujibu wa Waziri Ummy ni kuwa Mradi huo utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 100(sawa na Shillingi Bilioni 235 za Kitanzania)ambapo zitatumika kujenga Daraja la Jangwani na kuboresha Mto Msimbazi.
Aidha Mhe Ummy ametaka utekelezaji wa mradi huu chini ya Serikali ya Awamu ya 6 kuongeza kipengele cha kujenga Soko jipya la Jiji la DSM ambalo pia litaweza kuwa na sehemu maalum ya kuchukua takribani Machinga 10,000 na kufanya dhana ya kuboresha hali ya Masoko na Ufanyaji biashara kwa Machinga katika Jiji la DSM kuimarika zaidi.
Waziri Ummy amemtaka Katibu Mkuu wa TAMISEMI kuhakikisha Utekelezaji wa Mradi huu wa Uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi unaanza haraka ili tija yake itimie pasipo urasimu uliozoeleka.
Utekelezaji wa Mradi huo utafanya umaarufu wa Mto Msimbazi katika kuleta mafuriko kufurika na kufanya kuwa mto pendwa na wenye kutegemewa katika kupitisha maji kuelekea Bahari ya Hindi.
Sambamba na Wataalam Kikao hiki cha mkakati pia kimehudhuriwa na Mhe Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa DSM na Mh Mussa Azan Zungu, Mbunge wa Ilala.

Post a Comment