BARUA TOKA KWA MUNGU

Tumwamini nani? 
Hili ndilo swali linaloulizwa na karibu kila mtu hapa duniani. Ni nani asemaye ukweli. Kila mahali 
umejaa udanganyifu, dhuluma, rushwa, uonevu, vita, n.k. Tunatoka wapi? na tuko wapi? na tunakwenda wapi? Ni nani anayeweza kutuambia 
ukweli? Kwa bahati nzuri Mungu, aliyeumba vitu vyote, anayejua kila kitu, na anayeweza kila kitu, ametuandikia barua ya kututoa mashaka. Mungu mwenyewe anajibu maswali yetu yote katika  barua hiyo. Barua hiyo inaitwa Biblia. Biblia siyo mkusanyiko wa mawazo ya wanadamu. Waandishi wake waliongozwa na Roho Mtakatifu.

1. Biblia yenyewe inajishuhudiaje?
“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa 
kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.” 2 Tim. 3:16.
“Unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa
Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2 Pet. 1:21. 
“Maandiko hayawezi kutanguka.” Yn. 10:35. Biblia inajishuhudia kuwa imevuviwa, iliandikwa na watu walioongozwa na Roho Mtakatifu, na haiwezi kutanguka wala kukosolewa.

2. Je, Mungu ana uwezo gani unaomfanya kuwa mkuu kuliko miungu mingine? 
“Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; Mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.” Isa. 46:9-10.

3. Ni sehemu zipi za Biblia ambazo Yesu alizitumia katika mafundisho yake? 
“Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika Maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye 
mwenyewe.” Lk. 24:27. Torati ya Musa, yaani vitabu 5 vya kwanza katika Biblia. Manabii, yaani, Isaya, Yeremia, Ezekieli, Yoshua, 
Samweli, Wafalme, Waamuzi na manabii wadogo 12. Maandiko ya Agano la Kale yamegawanywa katika sehemu kuu tatu - Torati, Zaburi, na Manabii.

4. Je, Agano la Kale linazungumza habari za nani? Yesu akajibu, akawaambia, “Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa 
milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.” Yn 5:39. “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno 
yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.” Mdo.24:44. Zingatia: Wakati wa Yesu, Agano Jipya lilikuwa halijaandikwa. Maandiko yaliyokuwapo ni Agano la Kale peke yake.

5. Kwa nini mambo yaliyowapata wazee wa zamani yaliandikwa? 
“Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.” 1 Kor. 10:11. 
“Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.” Rum. 15:4. Mungu alitegemea kwamba, kwa kujifunza matukio ya Biblia, tungeweza kuuelewa vizuri zaidi upendo wake 
na namna anavyojishughulisha na wanadamu.

6. Je, kujifunza Maandiko kunatusaidiaje? 
“Na ya kuwa tangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate 
wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” 
2 Tim. 3:15,16,17. 

7. Je, Yesu alisema tunaweza kuupata wapi ukweli? 
“Uwatakase kwa ile kweli; Neno lako ndiyo kweli.” Yn. 17:17. 
Wanadamu hawaujui ukweli na wengi wao hawajui kuuelezea. Ndiyo maana kuna taabu na shida nyingi 
zisizo na ufumbuzi. Biblia inasema, “Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo 
kweli itawaweka huru.” Yn 8:32.
ufanye agano na Mungu kwamba tutatumia njia hiyohiyo kuutambua ukweli.

13. Je, Biblia inaulinganisha na nini msaada tunaoupata kutokana na kujifunza Biblia?
“Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.” Zab.119:105.

14. Tutafanyaje ili tusitende dhambi?
“Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata Neno lako.” Zab. 119:9.
Je, Unabii unathibitishaje kama Biblia imevuviwa? Biblia inasema
“Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri
mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.”
Isa. 42:8,9. “Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu
mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yango.” Isa. 46:9,10  Utabiri wa Biblia juu ya mambo ambayo yangetokea
baadaye, unathibitisha uvuvio wa Biblia, mambo hayo yanapotokea.
Angalia mifano ifuatayo

A. Kuinuka na kuanguka kwa falme nne zilizotawala dunia:Babeli, Umedi na Uajemi, Uyunani na Rumi.
(Danieli 2,7,8.)

B. Koreshi kuwa Mpiganaji ambaye angeiteka Babeli.
“Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi (mtiwa mafuta) wake, ambaye nimemshika mkono
wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango
mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda
mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata- kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani,
na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam,
Mungu wa Israeli.” Isa. 45:1-3.

C. Baada ya kuangamizwa, Babeli isingekaliwa tena.
“Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.” “Haya! juu ya mlima usio na miti inueni bendera, wapazieni sauti zenu, wapungieni mkono, kwamba waingie katika malango ya wakuu.”
(Isa. 13:19,2). “Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwa-mwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.” Yer. 51:37..

D. Misri kutokuwa na amri tena kati ya Mataifa.
“Nami nitawarejeza Wamisri walio katika hali ya kufungwa, nami nitawarudisha hata nchi ya Pathrosi,
hata nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme duni. Utakuwa duni kuliko falme zote, wala hautajifunua
tena juu ya Mataifa; nami nitawapunguza, ili wasitawale
tena juu ya Mataifa.” Eze. 29:14,15. “Nami nitaikausha mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu
wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi,
BWANA, nimenena neno hili.” Eze. 30:12,13.

E. Majanga ya kushtua dunia na hofu kadiri tunavyoelekea siku za mwisho.
“Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya Mataifa wakishangaa
kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.” Lk. 21:25,26.

F. Kuporomoka kwa maadili katika siku za mwisho.
“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako na nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha,
wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.” 2 Tim. 3:1-5.

G. Unabii juu ya matukio katika maisha ya Yesu.
“Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika Maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye
mwenyewe.” Lk. 24:27. “Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha
kwa maneno ya Maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.” Mdo. 18:28.
Kwa kuwa wakati huo Agano Jipya lilikuwa halijaandikwa, ni wazi kuwa Maandiko yanayozungumziwa hapa ni Agano la Kale. Utabiri wa Agano la Kale juu ya Masihi ulikuwa dhahiri na ulitimizwa na Yesu wa Nazareti kiasa cha kumfanya Yesu mwenyewe na Apolo kuutumia  kuwathibitishia Wayahudi kuwa Yesu alikuwa ndiye 
Masihi.

Moja kati ya uthibitisho mkuu kwamba Biblia si kitabu cha  kawaida tu kilichoandikwa na watu wema, ni uwezo wake  wa kubadili maisha ya watu. Inaweza kumbadilisha mtu 
mwovu kabisa na kumfanya kuwa Mkristo mwaminifu.  Inaweza kumfanya mtu asiye mwaminifu, kutaka kurejesha  alichochukua, au kusahihisha uongo aliosema.
Ni uwezo gani wa ajabu ulio katika kitabu hiki  unaobadilisha kiajabu matamanio na makusudi ya watu? Ni  uwezo wa kufanya miujiza wa Roho wa Mungu anayefanya 
kazi kupitia kitabu hiki kutuonyesha Mwana–Kondoo wa  Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.
Je, ungependa kuielewa Biblia vizuri zaidi?  Je, utatenga muda maalum kila juma kwa ajili ya kujifunza 
Biblia?  Kwa kutambua kwamba Biblia ni barua ya Mungu inayokueleza mapenzi yake, je, unakusudia kuishi sawasawa 
na neno lake kama asemavyo katika Biblia?

Maamuzi yako ni                          

Ubarikiwe

No comments