AMKA NA BWANA LEO 25

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumapili, 25/07/2021.

*JE UMEJENGA JUU YA MWAMBA?*

*Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. 1 Wakorintho 3:11.*

▶️Watu walipokuwa wameketi kando ya kilima, wakisikiliza maneno ya Kristo, waliweza kuona mabonde na makorongo ambayo kwayo vijito vya milimani vilipita njia zake za kuingia baharini. Katika msimu wa joto mito hii mara nyingi ilitoweka kabisa, ikiacha tu mikondo mikavu na yenye vumbi. Lakini wakati dhoruba za wakati wa baridi zilipolipuka juu ya milima, mito ikawa na nguvu, mibubujiko yenye kusukasuka, wakati mwingine ikifurika katika mabomde, ikichukua kila kitu katika mafuriko yake yasiyoweza kupingika. Mara nyingi, wakati huo, vibanda vilivyowekwa na wakulima kwenye bonde lenye nyasi, ambavyo vilionekana wazi kuwa mbali na hatari, vilifagiliwa mbali. Lakini juu ya vilima kulikuwapo na nyumba zilizojengwa juu ya mwamba. Katika sehemu zingine za nchi kulikuwa na makazi yaliyojengwa kwa mawe peke yake, na mengi yake yalikuwa yamehimili dhoruba za miaka elfu. Nyumba hizi zilitengenezwa kwa kazi ngumu na shida kubwa. Hazikuwa rahisi kufikiwa, na eneo lake lilionekana kuwa si rahisi kufikiwa kuliko bonde la nyasi. Lakini zilijengwa juu yake bure-bila madhara yoyote.

▶️Wale wanaosikia na kutii maneno ya Kristo wanajenga juu ya mwamba, na dhoruba itakapokuja, nyumba yao haitaangushwa. Wao kwa imani katika Kristo Yesu watapata uzima wa milele. Wale ambao ni wasikilizaji lakini sio watendaji wa maneno Yake, wanajenga juu ya msingi wa mashaka ambao ni mchanga, na janga litawapata.

▶️Kama Adamu na Hawa wangeyatii maneno ambayo Mungu aliwaambia mwanzoni, wasingeanguka kutoka katika katika hali yao ya kwanza. Mwokozi wetu alikabiliana na majaribu katika hali ya nguvu, kali kuliko yalivyowasilishwa kwa Adamu, na silaha yake pekee ni ile ambayo iko karibu ya wote-Neno la Mungu. Shetani alipomjia Kristo katika udhaifu wake, na kumwambia atulize njaa yake kwa kugeuza mawe kuwa mkate, na hivyo kuthibitisha  kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu, Kristo alijibu, "Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. (Mathayo 4:4)....

▶️ *Tutakutana na mafundisho ya uongo ya kila aina, na kama hatufahamu kile Kristo alichosema, na kufuata maagizo yake, tutapotoshwa.*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE

No comments