MBOWE KUPEWA TUHUMA ZA UGAIDI, CNN YACHAMBUA
KAMATAKAMATA YA KATIBA MPYA NCHINI
TANZANIA SASA NI MJADALA WA DUNIA!
"Je, ni Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe
aliyekengeuka au kuna baadhi ya watu wenye
msimamo mkali wanaomshinikiza? Hili ni swali
lililoulizwa na Prof. Nic Cheeseman, Profesa wa
Demokrasia kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham,
Uingereza wakati akichambua kupitia CNN tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA,
Mheshimiwa Freeman Mbowe na kupewa tuhuma za UGAIDI, ambapo alikamatwa pamoja na viongozi wengine wa Chama hicho pamoja na Dkt. Azaveli Lwaitama.
Kukamatwa kwao, kunafuatia kukamatwa kwa
Askofu Mwamakula, Dkt. Lwaitama pamoja na
wafuasi na viongozi wengine wa CHADEMA tarehe 17 Julai 2021 na kuachiwa baada ya masaa 30 kufuatia kelele nyingi kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa nafasi yao kama wasomi na wanazuoni, Askofu Mwamakula na Dkt. Lwaitama walikuwa
wamealikwa na CHADEMA kutoa mada kuhusu
mambo ya Katiba katika Kongamano la Ndani mjini Mwanza ambalo lilizuiliwa na Jeshi la Polisi kabla hata halijaanza.
Walifuatwa katika Hoteli waliyokuwa wamefikia na kukamatwa pasipo hata kuelezwa sababu ya kukamatwa kwao.
NINI MAONI YAKO..?
Katiba huru ndio msingi,magaidi ni kina Makonda na Sabaya wake
ReplyDeleteSerikali itazame hili suala kwa macho 2 kabsaaa.tunachafuliwa wakati nchi yetu ni ya Amani