WATATU WASIMAMISHWA KUFUATIA KUWA NA TUHUMA
Muungano wa Tanzania alifanya ziara katika soko la Kariakoo, ambapo baada ya kutembelea na kufanya mahojiano na wafanyabiashara wa soko hilo aliagiza kusimamishwa kazi kwa Uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo chini ya Meneja Mkuu
wa Shirika hilo, Ndugu Hetson Msalale Kipsi.
Pamoja na kusimamishwa kazi kwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo Ndugu Hetson Msalale Kipsi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mheshimiwa Ummy A. Mwalimu (Mb.) amemuelekeza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI kuwasimamisha kazi wafuatao ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili
1. Ndugu Paul Ritoy - Meneja wa Fedha.
2. Ndugu Philip C. Nkupana - Meneja Mipango na Biashara.
3. Ndugu Donald Sokoni - Meneja wa Afya na Usafi.
Ikumbukwe kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI alifanya ziara katika Shirika la Masoko Kariakoo tarehe 22 Mei, 2021 na kuzungumza na wafanyabiashara na kupokea malalamiko yao, sambamba na kutembelea maeneo mbalimbali ya Soko hilo,bambapo aliahidi kuunda Tume Huru ya Uchunguzi.
Tume hiyo iliyoundwa ina Wajumbe kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Fedha nanMipango, Msajili wa Hazina, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Taasisi ya Sekta Binafasi Tanzania
(TPSF).
Taarifa ya Tume hii mara itakapokamilika itawasilishwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua zaidi.
Post a Comment