WATANZANIA WUHAN WAFANYA UCHAGUZI WA MWENYEKITI
Jumuiya ya Watanzania wanaosoma na kuishi Wuhan, wamefanya uchaguzi wa kiongozi wa juu wa Jumuiya hiyo (Mwenyekiti) ambapo katika uchaguzi huo Bi Zainab Aziz Jawad mwanafunzi wa masomo ya Famasia katika chuo cha Tonghji iliyoko Wuhan amechaguliwa kuongoza Jumuiya hiyo ya watanzania Wuhan.
Wuhan, yenye watanzania takriban 400 ilikuwa ni sehemu ambapo ugonjwa wa korona ilikoanzia na kuipa jiji hilo kutambulika kwa namna ya utofauti duniani kote.
Jumuiya hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Jacob Julius Rombo (JaJu) ambaye amameliza muda wake rasmi na kumkabidhi Bi Zainab Jawad siku ya jana tarehe 21 June 2021.
Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya hiyo ndugu Jacob JaJu amesema katika kipindi chake cha kiongoza Jumuiya hiyo amejifunza mambo mengi sana ya kiongozi na kubwa namna ya kustahimili masuala yanapokuwa magumu na kufanya maamuzi sahihi kwa kufuata taratibu zilizowekwa hususan ukiwa nchi za watu.
Ndugu JaJu, amesema anaamini Bi Zainab Jawad ataweza kuiongoza Jumuiya hiyo kwa mafanikio makubwa kwani anao uzoefu wa kutosha kutokana na ukweli kwamba alipata kuwa makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Post a Comment