WATUMISHI 74,437 WAPANDISHWA CHEO
Serikali imewapandisha madaraja watumishi wa umma 70,437 nchini huku ikitenga shilingi bilioni 300 kwa ajili ya mishahara mipya itakayoanza kulipwa kuanzia mwezi June 2021.
Hayo yamebainishwa leo June 21,2021 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengwera wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa Idara wa Utawala na Rasilimali watu katika Utumishi wa Umma.
Mchengerwa amesema kuwa taratibu zote za upandishaji zinaendelea na watumishi hao waliopanda vyeo watapata mshahara wa mwezi huu kulingana na madaraja yao waliyopandishwa
’Watumishi 70,437 waliopandishwa madaraja, jumla ya Sh. Billioni 300 Rais Samia Suluhu Hassani ametoa kwa ajili ya kuwapatia mishahara mipya inayoanza kulipwa mwisho wa mwezi huu, alisema Waziri huyo’’, amesema Mchengerwa
Waziri amesema kuwa watumishi 11,983 wenye malimbikizo serikalini watalipwa malimbikizo ya mishahara yao kwani wamekuwa wakiendelea na uchunguzi na kupitia madai yao.
”Serikali imetenga Sh. 23,781 bilioni kuhakikisha wanawalipa malimbikizo watumishi hao ambapo ofisi yake imeshafanya uchunguzi na kujiridhisha kwamba ni kweli wanadai malimbikizo yao”
Waziri Mchengelewa amesema kuwa Rais ameshatoa fedha hizo hivyo malimbikizo ya watumishi hao nao watalipwa mwisho wa mwezi huu.

Post a Comment