WATAKIWA KUFANYA KAZI BILA KUCHAFUA MAZINGIRA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.Selemani Jafo amesema kuwa Taifa linahitaji uwekezaji wa Viwanda ambavyo vinalinda na kuhifadhi mazingira yetu kwa manufaa ya Kizazi kilichopo na kijacho.
Jafo alisema hayo mjini Kibaha mkoani Pwani alipofanya ziara katika kiwanda cha Vunjo Afro Company kinachozalisha misumari kilichopo eneo la Misugusugu alipofanya ziara kujionea hali ya kimazingira.
Alibaini changamoto mbalimbali za kimazingira pamoja na kubadilisha jina la kiwanda bila kutoa taarifa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Aidha, waziri huyo aliwataka wenye kiwanda hicho kufanya uzalishaji bila ya kuchafua mazingira kwani Serikali inataka maisha bora kwa wananchi wenye afya bora na salama.
Alionesha kutoridhishwa na mazingira ya kiwanda ambapo ameahidi kutokifunga na amekipa wiki mbili kuhakikisha maji yanayotumika wakati wa uzalishaji hayatiririshwi kwenda kwenye mazingira.
Pia aliwataka watoe taarifa juu ya utupaji wa uchafu au vumbi linalobaki kutoka kwenye chuma baada ya kuzalisha.
“Vumbi litokanalo na chuma ni hatari kwa maisha ya binadamu na viumbe hai, ikiwa kama kiwanda mnashindwa kueleza kuwa hili vumbi mnalipeleka wapi basi kwa asilimia kubwa ni wachafuzi wa mazingira yetu na hamna huruma na wananchi juu ya Maisha yao bali mnaangalia masilahi yenu.
"Kutokana na kushindwa kujieleza vizuri natoa wiki mbili kwenu mnieleze wapi mnapeleka vumbi hili, niseme tu kweli sijaridhika na mazingira na mwenendo wa kiwanda hiki, tunataka uwekezaji lakini uwekezaji wenye tija kwa Taifa, hivyo NEMC hakikisha mnafanya ukaguzi na kutoa maelekezo kwa kiwanda hiki," alisema Waziri Jafo.

Post a Comment