Advertisement

Responsive Advertisement

UNWTO YAIKUBARIA TANZANIA KUWA WENYEJI MKUTANO UJAO

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii [UNWTO], kupitia mkutano wa siku tatu wa kujadili nchi za Afrika jinsi gani zitajikwamua kutokana na madhara ya janga la UVIKO 19 na Utalii unaofanyika mjini hapa, limeikubalia Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa masuala ya Utalii Bara la Afrika ambapo pia wameiingiza Tanzania kuwa nchi ya tatu itakayowezeshwa mradi mkubwa wa masuala ya Utalii.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro ambapo amebainisha kuwa, Ujumbe wa Tanzania umeweza kupata faida hizo mbalimbali sambamba na kupata uzoefu mkubwa ikiwemo pia kutangaza fursa za Utalii za Tanzania katika mkutano huo ambao una wadau wakubwa wa Utalii.

"Tumekutana nchi nyingi za Kiafrika, tumejadili mambo mengi, tumebadilishana uzoefu mkubwa tumepata mawasilisho mbalimbali kutoka kwenye makampuni yenye uwezo wa juu kabisa wa kutangaza utalii duniani.

Lakini pia tumepata fursa ya kufanya mikutano ya ana k
wa ana na wadau mbalimbali moja kati ya wadau hao ni Katibu Mkuu ambaye anayeshughulikia masuala yaUtalii wa Umoja wa Mataifa Bw. Pololikashvili, ambaye amekubali mkutano ujao wa Utalii Barani Afrika, ufanyikie Tanzania". Alisema Mhe. Dkt. Ndumbaro.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, Katibu huyo pia amekubali yeye mwenyewe binafsi kutembelea Tanzania na kuonana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa pamoja na wadau wa utalii kwa ajili ya kufanya maongezi juu ya mustakabali wa Utalii baada ya UVIKO 19.

Ambapo pia amesema wameweza kuomba na kukubaliwa kuiingiza Tanzania kuwa moja kati ya nchi tatu Barani Afrika ambazo zitapata mradi wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya Utalii.

Post a Comment

0 Comments