Tanzania imeendelea kung'ara ndani ya Bara la Afrika kwa kutangaza vyema vivutio vyake vya Utalii ambapo imeweza kuwa miongoni mwa nchi10 bora kwa mwaka wa tatu mfululizo, kuanzia 2017 hadi 2020.
Ripoti hiyo imetolewa mapema jana 14 Juni kwenye mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Utalii Duniani (UNWTO), kupitia kwa Mtaalamu wa utangazaji wa Utalii, Bi. Olga Nowak aliitangaza Tanzania kushika nafasi ya Saba ambayo inakuwa ni mara ya tatu.
Katika mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na Watalaamu wake kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi na vya kipekee ambavyo havipatikani mahali popote duniani isipokuwa Tanzania.
Katika kumi bora hiyo, Afrika ya Kusini imetajwa kushika nafasi ya kwanza ikifutiwa na nchi ya Misri katika utangazaji vyema ya vivutio vyake vya utalii.
Aidha katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa kuendelea kuongoza na kufanya vizuri katika sekta ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa UVIKO19 ambao umeikumba karibu Mataifa mbalimbali duniani kote.
Tanzania imekuwa na vivutio mbalimbali vinavyotamba Duniani ikiwemo mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi zenye vivutio vikubwa vya Wanyama kama Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Nyerere, Hifadhi ya Ruaha, Tarangile,l pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.
Katika hatua nyingine Tanzania kushiriki katika mkutano huo wa siku tatu, kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ndumbaro na wataalamu, imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususani viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali kwa kufanya vikao vya ana kwa ana na viongozi wanaoshiriki mkutano huo.
0 Comments