Advertisement

Responsive Advertisement

TB JOSHUA KUZIKWA JULY 11

Kanisa la Sinagogi la Mataifa Yote (SCOAN), limetangaza kuwa mhubiri mashuhuri wa Nigeria Temitope Balogun Joshua, ambaye ni Nabii TB Joshua atazikwa kanisani kwake huko Lagos mnamo Julai 11, zaidi ya mwezi mmoja baada ya kifo chake.

TB Joshua alifariki akiwa na umri wa miaka 57, Jumamosi Juni 5, 2021 na sababu ya kifo chake bado haijawekwa wazi.

Kulingana na taarifa ya SCOAN leo mchungaji marehemu angezikwa kwenye majengo ya kanisa lake katika Jimbo la Lagos.

Lakini, taarifa hiyo inasema kwamba Sinagogi itafanya ibada ya wiki moja kuanzia Julai 5 hadi 11.

Taarifa ya kanisa, "Tunajua mnafahamu kuwa baba yetu katika Bwana, Nabii TB Joshua, amechukuliwa nyumbani kuwa na Bwana. Tunataka kukuhakikishia kuwa hakuna kitakachozuia kazi ya Mungu katika The SCOAN kuendelea. Nabii TB Joshua anaweza kuwa hayupo mwilini lakini yuko rohoni.

"Hivi sasa tunajiandaa kwa ibada ya wiki moja kuanzia Jumatatu 5 hadi Jumapili Julai 11, 2021 kwa heshima ya maisha na urithi wa Nabii TB Joshua.

Post a Comment

0 Comments