Advertisement

Responsive Advertisement

RASMI BBC KURUDISHA HUDUMA ZAKE BURUNDI

Hakuna vipingamizi tena kwa BBC kufanya shughuli zake Burundi’, Mamlaka ya habari CNC imesema.

Mamlaka ya habari nchini Burundi , CNC ilisema shirika la habari la BBC World service sasa linahitaji kuwa na leseni mpya kufanya shughuli zake nchini Burundi.

“Hakuna vikwazo tena kwa BBC kufanya shughuli zake nchini Burundi”, mwenyekiti msaidizi wa CNC bwana Lurent Kagimbi aliviambia vyombo vya habari siku ya Jumatano.

‘’Hatahivyo BBC watahitaji kutuma maombi ya leseni mpya kwa sababu leseni yake ilifutwa’’, Bwana Kagimbi aliongeza.

BBC World Service ilifungiwa kurusha matangazo mwezi Machi, 2019 baada ya kipindi cha makala cha BBC Africa Eye kuibua siri ya wafungwa walioshikiliwa kwa siri na kuteswa katika maeneo ya huduma za usalama.

Serikali ya Burundi ilikasirishwa na makala hiyo na kusitisha matangazo ya BBC kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Desemba 2018 kabla ya kuifuta leseni yake nchini humo Machi 2019.

Serikali ya Burundi ilikataza matangazo au kutuma taarifa kutoka tangu wakati huo.

Vyombo vingine vya habari vya ndani na vya kimataifa (ikiwemo Voice of America) pia vilifungiwa kwa kuhusishwa na ripoti za ghasia za mwaka 2015 baada ya maamuzi tata yaliyofanywa na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kutaka kutawala kwa muhula wa tatu.

Baadhi ya vyombo hivyo vimefunguliwa tena baada ya rais Evariste Ndayishimiye kutoa muongozo mwanzoni mwa mwaka huu kwa mamlaka ya vyombo vya habari kujadiliana na vyombo vya habari vyote vilivyosimamishwa au kufungiwa ili kurudisha shughuli zao.

Bwana Ndayishimiye atasheherekea mwaka mmoja akiwa madarakani Ijumaa hii.

(Via;@bbcswahili)

Post a Comment

0 Comments