Advertisement

Responsive Advertisement

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI KWA WENYEVITI WANNE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 16 Juni, 2021 amefanya uteuzi wa Wenyeviti wanne (4) wa Bodi za Wakurugenzi kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Bw. Juma Alli Mohamed Muhimbi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Kabla ya uteuzi huo Bw. Muhimbi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Transparen Financial and Tax Consulting Services Lid wa Dar es Salaam.

Bw. Muhimbi anachukua nafasi ya Mama Anne Semamba Makinda ambaye muda wake umemalizika.

2. Amemteua Dkt. Edmund B. Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB). Dkt. Mndolwa anaendelea na wadhifa huo baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza.

3. Amemteua Prof. John Wajanga Aron Kondoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC). Prof. Kondoro anaendelea na wadhifa huo baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza.

4. Aidha, Mhe. Rais Samia amemteua Prof. Valerian Cosmas Kanyengele Silayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC). Prof. Silayo ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA).

Uteuzi wa viongozi hawa umeanza leo tarehe 16 Juni, 2021.


Post a Comment

0 Comments