TAKRIBAN WATOTO 51 WATEKWA NYARA

Takriban watoto 51 wametekwa nyara  katika ghasia ambazo zimeua maelfu ya watu na wengine wamehama makazi yao katika mkoa wa kaskazini uliokumbwa na uasi wa Kiislam, lakini wafanyakazi wa misaada wanasema idadi halisi ya utekaji nyara inaweza kuwa kubwa zaidi.

Vikundi vyenye silaha nchini Msumbiji vinazidi kuwateka watoto kama mbinu ya vita, na kuwaweka waathiriwa katika hatari ya unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za mapema na kutumiwa kama wapiganaji katika mzozo unaozidi kuwa mbaya nchini humo, vikundi vya misaada vimesema Jumatano.

No comments