• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / Habari / SOMO LA MICHEZO LATAKIWA KUANZIA SHULE ZA AWALI

    SOMO LA MICHEZO LATAKIWA KUANZIA SHULE ZA AWALI

    Bisaya Raphael June 09, 2021 Habari
    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(Mb) ameelekeza ufundishaji wa somo la Michezo uimarishwe kuanzia shule ya awali, msingi, sekondari na vyuo ili kujenga hali ya kujiamini na kuwa mahiri kimwili na kiakili.

    Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa ameyasema hayo Jana wakati akifungua mashindano ya michezo na taaluma yajulikanayo kama UMISSETA na UMITASHUMTA yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

    Ameeleza michezo ni muhimu zaidi kwa makuzi na maendeleo ya taaluma ya watoto na vijana na ina mchango mkubwa katika kuimarisha afya ya mwili na akili.

    "Watafiti wamethibitisha kuwa michezo kwa madarasa ya awali kwa maana ya miaka 3 – 6 ni muhimu zaidi katika kuongeza uwezo wa mzunguko wa damu katika ubongo (kuongezeka kwa mishipa ya damu) na maendeleo ya afya na makuzi ya watoto kwa ujumla wake hivyo ni vyema tukajikita kumjenga mtoto huyu kuanzia kwenye Ngazi ya awali,"amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

    Ameongeza "Bila shaka sote tunaelewa kuwa binadamu hawezi kuwa na akili bora kwenye mwili dhaifu na Afya Bora inaweza kujengwa vizuri zaidi kwa kushiriki katika michezo hivyo tujikite katika kutengeneza vizazi vitavyokua na mahiri kwenye michezo wakati wote maisha yao."

    Majaliwa alibainisha kuwa katika siku za hivi za karibuni kumekuwepo na mafanikio makubwa ya vijana waliyoyapata kupitia Michezo na wengi ni wa hapa hapa Tanzania, kama vile Mbwana Samata.

    "Kwa hawa wachache wanatuonyesha picha kubwa ya namna ambavyo vijana wetu wengi wanaweza kufanikiwa kupitia michezo na sanaa tuongeze nguvu katika eneo hili,"amesema

    Aidha amesema Michezo na Sanaa vikiwekewa mipango sahihi vina nafasi kubwa ya kuchangia na kujenga uchumi endelevu wa Taifa na watu wake.

    "Sekta hizi ni fursa kubwa kwa vijana wetu kujiajiri, kuajirika na kuutambulisha utamaduni wetu ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu,"amesema.

    Amewataka wanafunzi wote wanaoshiriki katika mashindano hayo kutokuridhika na hatua waliyofikia kwenye mashindano hayo na yawe mwanzo wa kujiimarisha katika michezo na sanaa ili kulitangaza Taifa kupitia michezo na sanaa.
    #

    Related Posts

    Habari

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates