SOMO LA MICHEZO LIFUNDISHWE KWA WANAFUNZI

Waziri Mkuu @kassim_m_majaliwa ameagiza ufundishaji  wa somo la Elimu kwa Michezo ufanyike kwa wanafunzi wote katika Shule za Msingi na kuhamasisha wanafunzi wa shule za Sekondari kusoma somo hilo. 

Amesema kuwa hatua hiyo itawasaidia watoto kujenga moyo wa kujiamini, kuwa ubunifu, kuongeza mshikamano na umoja wa kitaifa  pamoja na kuimarisha afya ya taifa. 

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Juni 8, 2021) alipofungua mashindano ya michezo ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari  (UMISSETA) katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

Aliongeza kuwa vyuo vya ualimu vinapaswa kuimarisha masomo ya Elimu kwa michezo ili kila mhitimu aweze kutoka na ujuzi wa ufundishaji wa michezo na kutengeneza wataalamu wa kutosha ili kusaidia kukuza vipaji vya wanafunzi shuleni.

Aidha, Waziri Mkuu ameziagiza Mamlaka zote zinazosimamia na kuendesha michezo na sanaa katika shule ziwajibike kikamilifu kuhakikisha mashindano UMISSETA na UMITASHUMTA yanakuwa endelevu  “tafuteni mbinu mbadala za kupata washirika zaidi wa kugharamia michezo hii”.

Pia, Waziri Mkuu aliwaasa vijana kujiepusha na vitendo vitakavyokwamisha ndoto zao za kufanikiwa katika masomo na michezo kama vile matumizi ya madawa ya kulevya, uvivu na utoro shuleni.
officialhodari Asante waziri wangu kwa juhudi

No comments