SAMATTA BADO HAJAJIUNGA NA TAIFA STARS

Mshambuliaji Mbwana Samatta bado hajajiunga na kikosi cha timu ya Tanzania kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaochezwa Juni 13  saa 10:00 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Samatta ambaye ni nahodha wa Stars ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki lakini bado hajajiunga na timu hiyo.

Wakati huo huo kiungo Novatus Dismas anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Macabi Telaviv nchini Israel na yeye alikosekana katika mazoezi hayo.

.

No comments