RAIS SAMIA KUONGEA NA WANAWAKE JIJINI DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jumanne ya Juni 8, 2021 anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Wanawake wa Mkoa wa Dodoma.
Akitoa taarifa ya Mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa, kikao hicho kitafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo Jijini Dodoma kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Mhe. Mtaka ametoa wito kwa Wanawake wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kushiriki kikao hicho ili kupata fursa ya kumsikiliza Mhe. Rais Samia.
Aidha, amewataka Wanawake waliopo mikoa mingine ya Tanzania kufuatilia Mkutano huo wa Mhe. Rais Samia na Wanawake wa Mkoa wa Dodoma kupitia vyombo vya habari vikiwemo Vituo vya Luninga, Magazeti, Redio na Mitandao ya Kijamii.
Post a Comment