NENO KUU MAKAMBINI LEO 27

MAKAMBI JIJI LA TANGA
SOMO: KUWAJALI WENGINE
MCH: ERASTO NZUMBI
Trh 27 June 2021
Huduma Kuu Mchana

Jizoeze kutembelea wagonjwa mara unapopata taarifa zao wala usipende kutembelea misiba yao

2 Samweli 13:14-19
✓Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye.

✓Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako.

✓Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza.

✓Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake.

✓Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake.

✓Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti.

Ni wajibu wetu kuwatembelea wagonjwa. 

Elisha anaposhikwa na ugonjwa ...mfalme anamtembelea na kumtia moyo.

Yakobo 1:26-27......
✓Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.

✓Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

Wajibu wetu ni kuwa na Dini iliyo safi yenye kugusa mahitaji ya watu.
Mtu mmoja alisema "thamani yako inatengenezwa na watu wengine".

......Pandikiza tabia ya kuwapigia watu simu na  kuwajulia hali na kuwatia ❤️ moyo .

....Tembelea wagonjwa wanaweza kuongeza maisha.

.......Hata watu wema wanapatwa na matatizo. Mfano ni Elisha anaugua na akatiwa moyo na mfalme. Hata watumishi wa Mungu wataugua.

.....Bado tunaweza kuaptwa na shida lkn pamoja na Yesu tutakuwa salama.

Ugonjwa na matatizo na shida visiwe vizuizi vya kutomfanyia Mungu kazi. Kuna watu ambao watamfanya Mungu wa kwanza ata wakiwa ktk magumu na magonjwa.

Zoea kumfanyia Mungu kazi hata katika nyakati ngumu.

Jizoeze kutembea na silaa zako zote. Elisha alikuwa na uta na mshale wake.
✓Silaa yetu ni 
Maombi
Neno la Mungu n.k.
✓Pamoja na Yesu tutakwenda zaidi ya kawaidi. 

Waefeso 6:10-13
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.

Ktk ya changamoto zote vaeni silaha zote za vita kwani pamoja na Yesu ushindi ni hakika. 

Tumia fursa yako vizuri, nafasi yako vizuri wala usikate tamaa . Pambana tu kwani pamoja na Yesu ushindi ni hakika.

Barikiwa Sana

No comments