MIRADI 93 IMESAJILIWA KUTOKA SIKU 100 ZA RAIS SAMIA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika kipindi cha siku 100 za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imesajili miradi 93 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.6 ambayo itaingiza ajira zaidi ya 24,600 kwa vijana.

Amesema kuwa hatua hiyo inatoa alama kwa wawekezaji wa nje kwamba kwa sasa urasimu katika sekta ya uwekezaji unaendelea kupunguzwa katika maeneo ya usajili wa makampuni pindi muwekezaji anapokusudia kuja kuwekeza nchini.

Waziri Mkuu ameyasema leo (Jumapili, Juni 27,2021) alipofungua Kongamano la siku 100 za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan lililofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Ametumia fursa hiyo kutaja miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha siku 100.

Amesema mbali na miradi hiyo, pia Mheshimiwa Rais amefanya jitihada kubwa ya kuondoa tozo 232 zilizokuwa zinawakwaza wafanyabishara. “Tozo hizi zimeondolewa ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao hapa nchini.”

“…Na haya yote ni katika kuongeza mzunguko wa fedha kwa Watanzania ambao wanashiriki katika shuhguli mbalimbali za kuimarisha uchumi wao.”

Waziri Mkuu amesema katika kufanya kazi zake, Mheshimiwa Rais Samia ameendeleza mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi jirani ambapo ametembelea nchi za Kenya, Uganda na Msumbiji kwa lengo la kuimarisha urafiki na Mataifa ya jirani. Pia amepokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni alama ya mshikamano.

Amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia ameendelea kupanga mipango ya ujenzi wa miradi mipya katika siku 100 za uongozi wake ikiwemo kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa reli ya kimataifa kipande cha kutoka Mwanza mpaka Isaka, ujenzi wa meli mpya nne na ukarabati wa meli kongwe moja.

"Meli hizi zimewekwa katika maeneo yote, ziwa Victoria tuna meli moja ambayo ina uwezo wa kubeba tani 3000 za mizigo itakayotoa huduma kati ya Tanzania, Kenya na Uganda, pia meli nyingine ya MV Umoja ambayo awali ilikuwa inakwenda Uganda nayo inakarabatiwa"

Waziri Mkuu ameongeza kuwa katika kipindi cha siku 100 za uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia ameanzisha

No comments