NENO KUU LEO 19
🎈KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.
🔵NENO KUU.
🔵TRH. 19/06/2021.
🔵MCH. MARK. WALWA MALEKANA.
🔵*SOMO: MAPOKEO DHIDI YA SABATO.*
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:28
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 11:29
Jana tuliangalia habari ya Uumbaji na namna alivyotupatia siku ya pekee ya Kumwabudu na Kumwenzi Mungu kama Muumbaji. Huyu ndiye tunayemwabudu kila wakati.
Kwanini watu hupumzika siku ya Jumapili?
Jumapili imetajwa mara nane katika Biblia(Agano jipya) mara sita huzungumzia tukio la kufufuka kwa Yesu.
Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
Mathayo 28:1
Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka.
Marko 16:1
Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;
Marko 16:2
1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Luka 24:1
Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
Yohana 20:1
Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.
Yohana 20:2
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Yohana 20:19
Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.
Marko 16:9
Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia.
Marko 16:10
Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki.
Marko 16:11
Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba.
Marko 16:12
Mafungu haya yote huonyesha Yesu alilifuka siku ya kwanza ya juma.
Je, siku ya Jumapili ndiyo ya kwanza katika juma? Katika Biblia ya Kiswahili cha kisasa Habari Njema. Luka 24:1.. Siku ya Jumapili... Mathayo 28:1(Biblia Habari Njema) Jumapili alfajiri.....
Katika uumbaji ndiyo siku ambayo Mungu alianza kuumba.
Mafungu mawili mengine ni haya:
Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
Matendo ya Mitume 20:7
Kwanini usiku?
Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena.
Matendo ya Mitume 20:25
Biblia inasema Jumamosi jioni...(Habari Njema)
Fungu lingine la pili ni hili:
Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
1 Wakorintho 16:2
Hayo ndiyo mafungu ya Biblia kuhusu siku ya kwanza ya juma yaani Jumapili.
Katika historia ilikuwa desturi yao wapagani kulisujudia jua kama mungu wao hapa kilikuwa kipindi cha utawala wa Warumi na hawa walikuwa Warumi wapagani. Ndiyo maana huitwa Sun-Day.
Kanisa la mitume lilitunza sabato hadi lini? Sabato ilitunzwa kwa Miaka 300 hadi kusulibiwa kwa Kristo. Hata katika karne ya 4 bado ilitunzwa.
Je, badiliko lilitokeaje? Kanisa la Kikristo lilibadilishwa polepole bila wao kujua.
Sabato siyo siku ya Wayahudi bali ni ya BWANA mwenye Heshima kubwa.
Hivyo Jumapili ni siku aliyofufuka Yesu, hivi ndivyo Neno lisemavyo, mengine yaliyofuatwa ni mapokeo ya wanadamu. Lakini kwa Neno la Mungu ukweli umebaki palepale.
Wito kwako na Kwangu,
Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
Matendo ya Mitume 5:29
*IMETUPASA KUMTII MUNGU KULIKO MWANADAMU.*
SIKU YA SABA NDIYO SABATO KWA MUJIBU WA HISTORIA NA NENO LA MUNGU.
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
🙏🙏🙏🙏
Post a Comment