AFYA NA KIASI LEO 19

*KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.*

*AFYA NA KIASI.*

TRH. 19/06/2021.

*SOMO: VITOBO VYA MIFUPA.*

Huu ni ugonjwa ambao mifupa hutobokatoboka, na husababishwa na upungufu wa chokaa katika mifupa(calcium)

Pia husababishwa na:

1. Chakula chenye protini nyingi.

2. Kukosa mazoezi. Ambapo Hupelekea mifupa kupungua na kusinyaa.

3. Kutumia pombe, sigara, chai, energy drink. Na vingine vingi kama soda ya cocacola nk.

4. Kwa wamama ambao tayari hawawezi kuzaa yaani umri umeshapita, mifupa huweza kupungua.

Namna ya kuzuia ugonjwa huu:

Jipatie Vitami D. Ili mifupa iwe na nguvu hakikisha unapata mwanga wa jua kwa dakika 40 kwa siku. Epuka pia kufungia watoto ndani pindi wazaliwapo mweke nje, vinginevyo anaweza kupata matege kwa kukosa mwanga wa jua.

Usitumie hivyo yaani vinywaji kama vile pepsi, coca, energy nk.

Hivyo tumia kinywaji cha Machungwa unaweza kutumia machungwa kumi kwa siku hii itadumu kukuimarisha na mifupa yako kupata nguvu na kuimarika.

Ugonjwa huu huwapata watu kuanzia miaka 45+. Na hupelekea mgongo kupinda, maungio ya mwili kukosa nguvu.

*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*

chirongemagai74@gmail.com
🙏🙏🙏🙏

No comments