MUONGOZO WA KUSOMA BIBLIA LEO 2

LESONI, JUNI 2

SOMO: “KULIKUZA JINA LAKO” 



"Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka" (Mwanzo 12:2). 

Katika Mwanzo 12:2, Mungu anaahidi kulifanya jina la Abramu liwe kubwa, yaani, atamfanya awe mashuhuri. Kwa nini ni shauku ya BWANA kumtendea hivyo kila mwenye dhambi, pasipo kujali utii au uaminifu wake? Ni nani anayestahili jina “kuu”? (Soma #Warumi 4:1—5#, #Yakobo 2:21—24.#) Je Mungu alimkirimia Abramu ukuu na umashuhuri kwa faida yake binafsi, au iliwakilisha kitu zaidi ya hapo? Elezea.

Linganisha #Mwanzo 11:4# na #Mwanzo 12:2.# Ni nini tofauti kubwa kati ya hayo mawili? Ni kwa jinsi gani moja huwakilisha “wokovu kwa matendo” na nyingine “wokovu kwa imani”?



Mpango wa wokovu unategemea kazi pekee aliyoitenda Kristo kwa niaba yetu, hata hivyo, sisi wanufaikaji wa neema ya Mungu, tunahusika. Tunalo jukumu la kushiriki; uhuru wetu wa kuchagua una kipaumbele kikuu. Onesho la zama zote, pambano baina ya Kristo na Shetani, bado linaendelea ndani yetu na kupitia kwetu. Wanadamu na malaika wanachunguza kwa makini kuona nini kilichotupata katika pambano hilo (#1 Kor. 4:9#). Hivyo, vile tulivyo, kile tusemacho, kile tutendacho, japo tunadhani hakuna umuhimu nje ya mazingira yetu haya, inao mguso utakaoleta athari katika ulimwengu mzima. 



Kwa maneno yetu, matendo yetu, mitazamo yetu tunaweza kufanikiwa kumletea utukufu BWANA, ambaye ametenda makuu kwa ajili yetu, au tunaweza kuleta aibu kwake na kwa jina lake. Hivyo, pale Mungu aliposema na Ibrahimu kuwa atalikuza jina lake, hakuwa analizungumzia jina hilo kwa jinsi ambavyo dunia inachukulia umashuhuri. Kile kifanyacho jina kuwa mashuhuri machoni pa Mungu ni tabia, imani, utii, unyenyekevu na upendo kwa wengine, sifa ambazo japo zaweza kuheshimika hapa duniani, siyo vigezo vya kumfanya mtu duniani apate kuonekana ni mkuu.



Tafakari wanaume na wanawake walio na majina makuu katika ulimwengu wa leo —waigizaji majukwaani, wanasiasa, wasanii, matajiri, na kadhalika. Ni mambo gani katika watu hawa ambayo huwafanya wawe mashuhuri? Pambanisha hao na ukuu wa Ibrahimu. Hii hutuambia nini kuhusu vile dhana ya ukuu ilivyopotoshwa hapa duniani? Ni kwa jinsi gani dhana hii ya kidunia kuhusu ukuu imetuathiri pia sisi wakristo wa leo katika kutathmini ukuu halisi?

No comments