MALISA AUKOSOA UTEUZI WA KENANI KIHONGOSI

Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM iliyoketi leo mjini Dodoma ikiongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan imemteua Kenani Kihongosi kuwa Katibu Mkuu mpya wa UVCCM Taifa. Kihongosi anachukua nafasi ya Raymond Mangwala ambaye alipoteza sifa za kuendelea kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.

Hii ina maana kuwa Kihongosi kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa UVCCM "automatically" amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mkuu wa wilaya ya Iramba kama ilivyokua kwa mwenzie Mangwala. Hii ni kwa sababu sasa atakua mtendaji mkuu wa umoja huo wa vijana ndani ya CCM. Nafasi ya DC wa Iramba itajazwa baadae.

Hapa naliona tatizo kidogo kwa washauri wa Rais ndani ya chama chake na ndani ya serikali. Ni kama wanapishana. Washauri wa mama Samia ndani ya serikali waliona Kenani anafaa kuendelea kuwa DC, lakini aondolewe Arusha apelekwe Iramba.

Kenani akaripoti Iramba na kuapishwa hapo jana. Kabla hajakaa ofisini na kabla lori lililobeba mizigo yake halijafika Babati, washauri wa mama Samia kwenye chama wanamwanbia Kenani aje Dodoma kuwa Katibu mkuu wa UVCCM.

Kwanini hii "correlation" ya chama na serikali haikufanyika mapema ili Kenani aripoti moja kwa moja UVCCM badala ya kwenda Iramba na kuweka rekodi ya kuwa DC wa siku moja? Najua mama anasuka "safu" yake ndani ya chama, lakini kuna haja ya washauri wa Rais ndani ya serikali na wale wa ndani ya chama kushirikiana ili kuepusha migongano kama hii.!

----- Malisa GJ.✍

No comments