MALISA AIBUA MAZITO YA SABAYA

MALISA;
Alipofika ofisini, wakaongea na akamuonesha nakala za vibali. Sabaya akatoka ofisini na kumuacha ndani. Aliporudi akamnyang'anya simu zote, na kumuamuru akae chini. Akaita mabaunsa wake, wakamvua viatu na mkanda na kumpeleka rumande.

Taarifa za kukamatwa kwake zikafika kwa viongozi mbalimbali wa serikali. Wizara ya ya viwanda na biashara ikatoa tamko kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kwa mujibu wa sheria. Wizara ya uwekezaje, ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali, Shirika la viwango (TBS), pamoja na ofisi ya BRELA wakaingilia kati na kueleza kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kihalali.

Kesho yake Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro akafanya press na kutoa ufafanuzi kuwa kiwanda hicho kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Taarifa hiyo ikaeleza kuwa mwezi April kiwanda hicho kilipewa stika za 200M na kiliweza kuhuisha stika za 93M. Pia kwa siku chache za mwezi May (kabla hakijafungwa) kilikua kimehuisha stika za 13M.

Taarifa ya TRA ikaeleza kuwa kiwanda hicho hakijawahi kuwa na mgogoro wowote na serikali wala hakijawahi kujiendesha bila kuwa na vibali. Ikatangaza kukifungulia kiwanda hicho na kukiruhusu kiendelee na uzalishaji.

Media zote zilizoripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa zilialikwa kwenye Press ya TRA ili ziujulishe umma kwamba taarifa ya Sabaya haikua sahihi, na kwamba kiwanda hicho kimeruhusiwa kuendelea na uzalishaji.

Lakini Sabaya akazuia media hizo zisiripoti taarifa hiyo ya TRA. Ni ITV pekee walioamua kusimama katika misingi ya taaluma na kutoa ufafanuzi kwa umma. Media nyingine zilizoripoti ziliamua kusimama na Sabaya. What a shame?

Tayari Jeff ameshaenda TAKUKURU kuwasilisha ushahidi wake. Pia atawasilisha malalamiko Baraza la habari nchini (MCT) ili media zilizomchafua na zikakataa kumsafisha zichukuliwe hatua, kwa sababu habari ya kiwanda hicho kufungwa imeathiri mauzo kwa kiasi kikubwa

No comments