HII NCHI INA WASHAMBA WENGI SANA-MALISA GJ

Hii nchi ina washamba wengi sana waliopewa madaraka. Just imagine huyu ni mkuu wa wilaya akimtishia mwananchi wake kwenye group la whatsapp. @simon.odunga.3, Mkuu wa wilaya ya Rorya akimtukana na kumtishia kada wa Chadema @wamajiwa_mteute kwa sababu tu Wamajiwa alimkosoa kuhusu kunyanyasa wapinzani Rorya.

Odunga ni miongoni mwa watanzania wachache walioaminiwa na Magufuli wakapewa nafasi za uongozi. Leo anatishia kubana wananchi wake korodani. What a shame? Tena anaandika kwenye group la whatsapp openely bila hata kujali. Kiongozi ni pamoja na kuwa na busara. Huwezi kutamka maneno ya hovyo hivi hadharani halafu ukajiita kiongozi.

Eti huyu ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya? Mtu anayemwakilisha Rais katika wilaya? Mtu asiye na busara hata za kuazima.

Kama DC umeona mwananchi wako amekosea kwanini usiagize vyombo usalama vimkamate na kumfikisha mahakamani ili akipatikana na hatia afungwe? Instead unatishia kumdhuru bila kujali kuwa wewe ndio msimamizi wa sheria katika wilaya yako.

Je umeshadhuru wangapi hadi sasa? Kama unaweza kutamka haya hadharani, that means sirini unafanya makubwa zaidi ya haya. Who knows? Nyie ndo akina "Sabaya" mliokosa promo sio?

Anyway, tunamuachia mama Samia Suluhu  Hassan aamue kama ataendelea na kikundi hiki cha wakora kinachotishia kudhuru wananchi hadharani, au atatafuta wasaidizi wengine wenye kuheshimu sheria za nchi.

Ni muhimu pia uchunguzi ufanyike kwa DC huyu, yawezekana alishadhuru wengine. Akipatikana na kesi ya kujibu afikishwe mahakamani. Tujenge jamii ya viongozi wanaoheshimu sheria za nchi, na sio kujiona wao ni miungu watu wanaoweza kumnyanyasa yeyote wanayetaka.!

No comments