MALEKEZO YA SEKTA YA ELIMU KWA MAKATIBU TAWALA

Kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mradi mpya wa Elimu Sekondari (Sequip) na tunaanza na Ujenzi wa shule za Sekondari za Wasichana 26
kwa kila Mkoa kwa pamoja mkubaliane sehemu sahihi ya kujenga shule hiyo.

Kupitia mradi huo pia (Sequip) tutajenga shule Mpya 1000 kwa sasa tuna kata 719 ambazo hazina shule hivyo tutajenga
kwenye kata hizi na zile ambazo zina shule lakini zina wanafunzi wengi.

Kusimamia kikamilifu Ujenzi wa Madarasa ya kuwapokea wanafunzi cha kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2022 tusisubiri zimamoto na tayari tumeshatoa makisio.

Tukasimamie ukusanyaji wa Takwimu sahihi za Elimu ili zitusaidie kufanya maamuzi na kupeleka rasilimali ni aibu kuona shule ya matope kwenye vyombo vya habari wakati tuna maafisa elimu katanwanaotakiwa kutoa taarifa hizi.

Tuzisimamie Halmashauri katika kuhakikisha kwamba wanaandaa mazingira wezeshi kwa walimu wa Ajira mpya watakaoajiriwa hivi karibuni.

Kusimamia mfumo wa Uhamisho wa Walimu
utakaoanza kufanya kazi Julai 2021.

Kuhamasisha wananchi kutumia namba za kituo
cha huduma kwa wateja kuwasilisha kero zao.
Tumeelekeza kila ofisi ya serikali ibandikwe namba ya kituo hiki.

No comments