UFAFANUZI CHAGUZI ZA KIDATO CHA TANO&VYUO

KUTOKA WIZARA YA TAMISEMI;
Miongoni mwa malalamiko yaliyopo kwenye ujumbe huo ni wasiwasi wa kuwa machaguo
ya wanafunzi hayazingatiwi na wanafunzi wanapangiwa shule na vyuo ambavyo hawajachagua. 

Aidha, mwandishi wa andiko hili pia amelaumu kuhusu wanafunzibkupelekwa kwenye tahasusi ambazo sio chaguo lao. OR TAMISEMI inapenda kutoa ufafanuzi wa masuala haya kama ifuatavyo:

• Wanafunzi wote walitakiwa kuweka machaguo matano ya tahasusi (combination) za kidato cha tano pamoja na kuweka machaguo ya vyuo kwa ambao watakosa nafasi za kidato cha tano pamoja na wale ambao wanapenda kwenda kwenye vyuo vya kati moja kwa moja. Ukweli ni kwamba wanafunzi wamepagwa kulingana na machaguo yao (Chaguo la kwanza hadi la tano) kulingana na ufaulu wake sifa za kuchaguliwa kwenye tahasusi husika. Hivyo kuna wanafunzi wamechaguliwa kujiunga kwenye tahasusi ambayo ni chaguo lake la tano
kulingana na ufaulu wake. Aidha kama chaguo lake la kwanza ni kidato cha tanobna Cut off Point inaruhusu atachaguliwa kidato cha Tano na kama hairuhusu atapangiwa chuo kwa kadiri alivyochagua.

• Mwanafunzi aliyekosa machaguo yake kutokana na ushindani unaodhibitiwa na nafasi zilizopo kwa mwaka husika, huchaguliwa kwenye tahasusi nyingine yoyote aliyofaulu huku kipaumbele kikienda kwa zile tahasusi za Sayansi. Wanafunzi
wanaochaguliwa kujiunga na fani mbalimbali za vyuo, huchaguliwa kwa utaratibu huo huo wa kuzingatia machaguo yao wenyewe ikifuatiwa na fani nyinginezo endapo wamekosa machaguo yao kulingana na nafasi zilizopo.


. Ikumbukwe kuwa OR TAMISEMI imeweka mfumo wa kumruhusu mwanafunzi kubadilisha machaguo yake ya tahasusi baada ya matokeo ya mitihani kutoka ili aweze kuchagua tahasusi kulingana na ufaulu wake. Jambo hili limesaidia
sana wanafunzi kuweza kuchagua tahasusi inayoendana na ufaulu wake.

. Kabla ya mwaka 2018 kulikuwa hakuna nafasi ya kubadilisha machaguo ya tahasusi baada ya matokeo ya mitihani kutoka Utaratibu huu umekuwa ukifanyika kwa miaka mitatu sasa, mfano mwaka 2019 wanafunzi 36,268 walibadili machaguo yao Mwaka 2020 walikuwa 36,264 na Mwaka 2021 waliobadilisha ni wanafunzi 40.424. Mfumo wa Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga
na Kidato cha Tano na vyuo vya Ufundi hutegemea taarifa zilizoingizwa na kuhuishwa na Wanafunzi/Walezi/Wazazi, na sio kwa maombi mengine tofauti.

. Serikali imewezesha wanafunzi wengi iwezekanavyo kuendelea na masomo kupitia utaratibuu huu wa kuwapeleka kwenye vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wanafunzi ambao wamekosa nafasi ya kidato cha tano. Kabla ya mfumo huu wa kuwapangia wanafunzi wanaokosa nafasi za kidato cha tano moja kwa
moja chuoni mwanafunzi alilazimika kutafuta mwenyewe nafasi katika vyuo hivyo kwa kuomba moja kwa moja chuoni na hii iliwasababishia usumbufu na kuongeza gharama kwa wanafunzi, wazazi na walezi ikiwamo gharama zanfomu za maombi ya chuo.

• Ifahamike kuwa hakuna mwanafunzi mwenye ufaulu wa Daraja la kwanza aliyechaguliwa kujiunga na fani zilizotajwa kwenye waraka huo kama alivyobainisha Mwandishi huyo. OR TAMISEMI inaendelea na juhudi za kumtaka mwandishi huyo atoe index number za wanafunzi anaodai wamechaguliwa kwenye kozi ambazo haziendani na ufaulu wao mpaka sasa hazijafanikiwa ili kutoa ufafanuzi zaidi. Wananchi wote mnahimizwa kutoa taarifa zenye uhakika kwa jamii vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yoyote anayesambaza taarifa zenye kuleta taharuki kwa wananchi
Iwapo mwananchi anahitaji ufafanuzi wowote kuhusu Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kuingia Kidato cha Tano na Vyuo, wananchi mnakumbushwa kuwasiliana na kituo chetu
cha huduma kwa mteja kupata maelezo sahihi. Kituo chetu kinapatikana kwa namba za
simu: +255735-160210, +255262-160210 ama kuandika barua pepe kwenye anwani
yetu ya huduma@tamisemi.go.tz.

No comments