SERIKALI MBIONI KUTEKELEZA MRADI WA (LNG)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim, amesema Serikali ipo mbioni kuanza kutekeleza mradi wa kimkakati wa uzalishaji wa gesi asilia ya kimiminika (LNG) mkoani Lindi utakaogharimu dola za kimarekani bilioni 30.
Amesema kuwa Mradi huo ni moja ya mradi wa kimkakati ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepania kuutekeleza katika awamu ya sita ambao utakapoanza kutekelezwa itatumika kwa kipindi cha zaidi ya miaka 25.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi Juni 5, 2021) wakati wa mkutano na wadau wa maendeleo wa wilaya ya Lindi, katika ukumbi wa hoteli ya Sea View Mjini Lindi.
"Vile viwanja mlivyovichukua anzeni kuvijenga, mradi wa gesi asilia unakuja, nina amini mradi huu ukianza baada ya kukamilisha makubaliano, tutafika hatua nzuri, jiandaeni kutumia fursa hii" amesema.
Aidha, Waziri Mkuu amezitaka Halmashauri nchini ziongeze usimamizi kwenye sekta ambazo wananchi wanazitekeleza kila siku ikiwemo sekta ya kilimo na kuifanya moja ya agenda muhimu kwa kuwa watanzania wengi wanategemea kilimo katika kujipatia kipato.
"Halmashauri zetu nyingi watu wake ni wakulima, wafanyakazi ni asilimia tano tu na hata wafanyabishara ni asilimia ndogo, viongozi simamieni kilimo ili kiimarishe pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla”

Post a Comment