KUREJEA KWA HUDUMA YA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inapenda kuwajulisha wakazi wa Bagamoyo na Jiji la Dar es Salaam kuwa Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini umewashwa kwa ajili ya kurudisha huduma ya Majisafi.
Awali mtambo wa huo ulizimwa kwa saa 24 kuanzia tarehe 17.06.2021 hadi 18.06.2021 kupisha Matengenezo katika mfumo wa mtambo hali iliyopelekea ukosefu wa huduma kwa sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam.
Kufuatia kuwashwa kwa mtambo huo, huduma ya majisafi imeanza kurejea kwenye maeneo yaliyoathirika awali. Huduma itaendelea kuimarika kadiri maji yatakavyokuwa yakiongezeka katika mfumo.
DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokea.

Post a Comment