DAR KUFIKIA 100% UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI IFIKAPO 2022
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ametembelea na kuangalia kasi ya utekelezaji mradi wa usambazaji maji kutoka Bagamoyo hadi Makongo na kuwaahidi watanzania kuwa adha ya upatikanaji huduma ya maji kwa Jiji la Dar es Salaam kumalizika ifikapo 2022.
Ziara hiyo imelenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo unaohusisha ujenzi wa matanki makubwa ya kuhifadhi maji pamoja na ulazaji wa mabomba kwa umbali wa kilomita 1,426.
Akizungumza juu ya Utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Luhemeja amesema mradi unahusisha ujenzi wa matank matatu makubwa yakuhifadhi maji katika maeneo ya Vikawe, Tegeta ‘A’ na Bunju pamoja na ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma maji.
"Kazi zingine zitahusisha ujenzi wa mabomba makubwa ya kusafirisha na kusambaza maji yenye kipenyo cha kuanzia inchi 10 mpaka 20 kwa umbali wa km 23.38 pamoja na ujenzi wa mabomba ya kusambaza maji yenye kipenyo kwanzia inchi 3 hadi inchi 8 kwa umbali wa km 1,195" aliongeza Luhemeja.
Afisa mtendaji mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mkandarasi ana wajibu wa kuunganisha wateja zaidi ya 60,000 ili kumaliza changamoto za maji katika maeneo ya Bagamoyo, Mabwepande, Mivumoni, Madale, Wazo mpaka Changanyikeni ambapo mpaka sasa kazi imefikia asilimia 50.
“Mkataba huu tunagemea utakamilika mwezi Novemba na hadi sasa kazi inakwenda vizuri, kuanzia Julai,5 tutaanza kuunganisha wateja wa Bagamoyo ambapo tunategemea kuanza na wateja 3500 ambao wataanza kunufaika na mradi” aliongeza Mhandisi Luhemeja.
Mhadisi Luhemeja ameeleza miradi yote inayoendelea ni sehemu ya jitihada za Mamlaka za kuondoa changamoto ya maji Dar es salaam na kuahidi ifikapo 2022 DAWASA itatangaza kuisha kwa changamoto ya Maji Jijini Dar es salaam.
"Hadi sasa upatikanaji wa huduma ni asilimia 92 kwa Jiji la Dar es Salaam, haya ni mafanikio makubwa sana kwetu na tunahakikisha miradi hii ikikamilika itamaliza asilimia 8 iliyobaki " allimalizia Mhandisi Luhemeja
Kukamilika kwa mradi huu kutaenda kunufaisha wananchi wa maeneo ya Changanyikeni, Salasala, Kinzudi, Goba, Madale na Bagamoyo.

Post a Comment