KAYA NA FAMILIA

🔴SABATO NJEMA🔴
________________________

❣️KAYA NA FAMILIA.

❣️TRH. 11/06/2021.

MAMA, DEVOTHA SHIMBE.

❣️SOMO: KUJIFAHAMU KABLA YA KUTAFUTA MWENZI.

Kujifahamu ni jambo la pekee sana kabla hujamfahamu mwingine.( Johari window) ni kanuni nzuri ya kutumia, kuna sehemu ya wazi ambayo humaanisha watu wanakufahamu na wewe unawafahamu lakini lililojificha honyesha kuwa unavyojifahamu ndivyo wanavyokufahamu. Upande mwingine watu wanakufahamu hivyo ila wewe hujui kama ndivyo wanakufahamu na unaweza kuambiwa na watu wengine usikatae. Chumba cha mwisho kinaonyesha wewe hujui na wengine hawajui. Unaweza kupewa kazi utende ili wakuone kama unajua na hii ni kwa uwezo wa Mungu pekee.

Ninawezaje kujifahamu?

Kupitia staha yangu.

Uwezo wangu wa kiakili katika kutatua mambo.

Uwezo wa kutawala hisia zako na namna ya kuishi na watu wengine. Hisia zako zisiathiri mtu mwingine.

Nini maana ya staha?

Ni nanmna unavyojiona wewe mwenyewe kabla ya kuambiwa na watu wengine.

Aina za staha.

a) Staha ya juu. Akipewa kazi yoyote anaweza.

b) Staha ya chini. Yeye anashindwa kabla hajaanza.

Amini jinsi ulivyo kabla hujaambiwa na mtu. Jikubali kuwa hivyo ndivyo ulivyo. Mungu amekufahamu hata kabla hujaumbwa.

Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, 
Zaburi 139:14

Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; 
Zaburi 139:15

Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. 
Zaburi 139:16

Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake! 
Zaburi 139:17

Staha ya chini ni ugonjwa unaowasumbua wengi hasa wanawake. Mfano wanajikataa kwa kubadili majina, sura, nywele, maumbo ya miili yao hii ni kwa sababu ya kujikataa yaani hawajikubali.

Hata vijana wa kiume nao wamekuwa na ugonjwa huu pia.

Mabinti hawajikubali kimaumbile, mwili wake pia haukubali kabisa.

Akinenepa kidogo anakata tamaa, wengine kutokula ili wawe na miili midogo(miss) kuwa wembamba. Tulia kwa Yesu usijibadili.

Jiangalie mwenyewe, jiamini, jikubali hivyo ulivyo ndivyo. Jipe asilimia zako mwenyewe.

Staha ya chini huja kupitia uzoefu maishani uliopitia aidha mbaya mfano mahusiano yako na wazazi, au wazazi wenyewe hii inakufanya usijiamini. Hivyo wazazi msitukane watoto wenu.

Mtu mwenye staha ya chini hata maamuzi yake ni magumu. Ni vigumu kuamua mambo. Yuko tayari kukubaliana na mtu yeyote hata kama hafai huu ni ugonjwa.

Staha inaweza kubadilika endapo utabadili mtazamo wako tu. Hivyo badili mtazamo ilo uwe na staha ya juu.

Shida nyingine huja pale mtoto anapolazimishwa kufikia malengo asiyoweza ambapo akishindwa masomo hayo staha yake hushuka.

Kukosea kuoa au kuolewa hushusha pia staha yako.

Kujinenea mambo mabaya hushusha staha, huamini kuwa unachoambiwa hata kama ni jambo jema.

Wenye staha ya chini hawajiamini, hawajikubali, wana hasira, wana hofu.

❣️AFYA NA KIASI.

❣️TRH. 11/06/2021.

❣️SOMO: UGONJWA WA MOYO NA MISHIPA YA DAMU.

Ni ugonjwa ambao husababishwa na kuzibwa kwa mishipa ya damu na ile inayopitisha damu. Hivyo hupelekea damu kukwama na kuganda. Hivyo hii wakati mwingine hupelekea ugonjwa wa kiharusi.

Dalili za mshituko wa moyo:

Kichefuchefu, kukosa jasho, kizunguzungu, wasiwasi au kutokujiamini, kuzimia au kupoteza fahamu, kutapika, kukosa nguvu hizi zote ni dalili za mshituko wa moyo.

Watu wangeweza kuepukana na ugonjwa huu endapo wangebadili mtindo mzima wa maisha wanayoishi kupitia lishe.

Wakati mwingine mishipa ya damu huzibwa kutokana na utumiaji wa mafuta mengi mwilini na kwa sababu hiyo kupelekea ugonjwa.

Dalili nyingine ya mshituko wa moyo ni maumivu makali kifuani.

Sababu zake:

Uvutaji wa sigara huu huuwa wengi mno, kiwango kikubwa cha mafuta(lehemu) ni visababishi vikuu vya ugonjwa huu.

Afya ni uchaguzi wetu. Ugonjwa huu kabla ya miaka 80 shida ni kwetu wenyewe kwa kutojali afya zetu.

Sababu zingine ni kama vile uzito mkubwa wa mwili. Pombe, kunywa kahawa maana kahawa huaribu mfumo wa mapigo ya moyo.

Tuache kula kabisa chips kwa kuwa zina mafuta mengi ya ziada ambayo unapokula yanaenda kujaa mwilini na kuongeza uzito mkubwa na hatimaye ugonjwa.

Ni lazima upime ili ujue kuwa una ungonjwa huu au la!

Tiba yake pamoja na kuwepo vidonge na sindano lakini hizi haziponyi ila hupunguza ukali tu. Suluhisho siyo sindano au vidonge. Ajenda ni kupunguza kula vyakula vya mafuta. Acha pombe, kahawa, sigara, punguza chumvi ongeza matunda zaidi. Pima uzito kila wakati. Pia ufanye mazoezi ya kutosha.

MUNGU ATUBARIKI SOTE.
🙏🙏🙏🙏

No comments