KAMATI HAIKUBAINI UKWERI

TAARIFA KUTOKA YANGA;
Kufuatia kikao cha Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Yanga kilichofanyika Jumapili Mei 30, 2021, pamoja na mambo mengine kilipitia ripoti ya
Kamati huru iliyoundwa kuchunguza tuhuma zilizomkabili aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu, Wakili Simon Patrick.

Ripoti hiyo ya kamati huru iliyoongozwa na Wakili Raymond Wawa, haikubaini ukweli wowote katika tuhuma zilizoelekezwa kwa Simon,nna hivyo baada ya kujadiliana kwa kina, Kamati ya Utendaji imejiridhisha pasi na shaka kwamba Wakili Simon Patrick hakuwa na hatia katika tuhuma hizo zilizopelekea kusimamishwa kazi Novemba 18, 2020.

Wakili Simon, alisimamishwa kufuatia kikao cha Kamati ya Utendaji cha Novemba 17, 2020, hivyo basi kutokana na ripoti ya Kamati huru
kutomkuta na hatia yoyote, na kutokana na Kamati ya Utendaji kujiridhisha kwamba Simon hakuhusika kwa namna yoyote na tuhuma
zilizomkabili, Kamati ya Utendaji imemrejesha kazini wakili Simon katika nafasi yake ya Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama kuanzia
Mei 30, 2021.

Uongozi wa Yanga, unawaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wa Klabu kuendelea kumpa ushirikiano Wakili Simon Patrick katika
kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa maendeleo ya klabu ya Yanga.

No comments