GOLIKIPA PATRICK MATASI APATA AJALI
Mlinda lango wa kimataifa wa Kenya Patrick Matasi amelazwa hospitalini baada ya kupata ajali ya gari kwenye barabara ya Kapsabet-Nakuru huko Lessos, Nchini Kenya.
Kipa huyo wa zamani wa AFC Leopards kwa sasa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Kapsabet ambapo alikimbizwa, katika gari la wagonjwa (AMBULANCE).
Kulingana na jamaa yake Albert Mulanda, anasema Matasi bado anafanyiwa uchunguzi, kwani analalamika bado ana maumivu ya kifua.
Post a Comment