FAHAMU WALIOAPISHWA LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Juni, 2021 amemuapisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Razi Maxam Mhe. Kept. Mst. George Huruma Mkuchika aliyemteun tarehe 31 Machi, 2021 na amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa 11 aliowateua tarehe 29 Mei, 2021.
Hafla ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa huo imefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson.
Makatibu Tawala wa Mikoa walioapislwani Mhe. Balozi Batilda Salha Buriani (Shimango, Bw. Rodrick Lazaro Mpogolo (Kita), Bi. Dorothy Aidan Mwaluko (Sing), Dkt. Athumani Juma Kihamia Arusha, Mhandisi Mwanaisha Rajabu Tumbo
(Prand, Bw. Ngusa Dismas Samike (Mwanza), Bw. Hassan Abasi Rugwa Dar es Salam, Dkt. Fatuma Ramadhan Mganga (Dolom, Bw. Musa Ramadhani Chogero (Gent), Bi. Pili Hassan Mnyema (Tagal na Bi. Prisca Joseph Kayombo (Sim. Mhe. Rais Samia ameshuhudia Makatibu Tawala wa Mikoa hao pamoja na Wakuu wa Taasisi 4 aliowateua hivi karibuni wakila kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi. Wakını wa Taasisi hao ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinni CP. Camilius Wambura, Mkuu wa Kamisheni ya Fedha na Lojastiki wa Jeshi la Polisi CP. Hamad Khamis Hamad, Afisa Mtendaji Mkuu, Tume ya Ushindani wa Biashara Bw.
William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Dkt. John Kedi Mduma.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Rais Samia amewapongeza viongozi wote walioapishwa na amewataka kwenda kuchapa kazi kwa juhudi, maarifa, kuzingatia sheria na utu ili kutimiza matarajio ya wananchi kwa Serikali yao.
Amesema ameongeza uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa wanawake hadi kufikia asilimia 46 ya Makatibu Tawala wa Mikoa wote nchini kwa kuwa anaamini kuwa wana uwezo, hivyo amewataka kuonesha mfano bora wa uongozi katika Mikoa yao.
Mhe. Rais Samia amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza ipasavyo wajibu wao wa kuwa kiungo kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, kusimamia vizuri rasimali za umma hasa ukusanyaji wa mapato matumizi yake, kuhakikisha mapato yanayopaswa kuelekezwa katika shughuli za maendeleo na makundi maalumu yanapelekwa kamanilivyopangwa katika halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.
Ameonya dhidi ya vitendo vya baadhi ya viongozi kudharauliana, kubaguana, kurumbana na kugombana badala ya kushirikiana kusukuma mbele maendeleo ya Mikoa na taasisi wanazoziongoza pamoja na kutatua kero na malalamiko wananchi.
Pia, ametaka viongozi hao kwenda kushughulikia migogoro inayowakabili wananchinhususani migogoro ya mirathi ambayo inawaathiri zaidi wanawake, migogoro ya ardhi na ameonya kuwa hatavumilia kuona viongozi hao wanakuwa sehemu ya migogoro kutokananna kujimilikisha ardhi katika maeneo wanayoongoza.
Mhe. Rais Samia amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kushughulikia changamotonzinazowakabili watumishi wa umma, kusimamia uchumi vizuri ikiwa ni pamoja na kusimamia uendelezaji wa viwanda, kuvutia wawekezaji, kusimamia vizuri taasisi za Serikali zilizopo katika Mikoa yao, kusimamia kwa ukaribu miradi ya maendeleo
inayotekeleza katika maeneo yao na kushirikiana na wananchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika utekelezaji wa Ilani iliyoiweka Serikali madarakani.
Aidha, Mhe. Rais Samia amewaonya viongozi hao pamoja na viongozi wengine walioteuliwa katika nyadhifa mbalimbali kuacha vitendo kwenda Majimboni kufanya kampeni za chinichini za kutaka Ubunge na badala yake wawaache Wabunge wa Majimbo hayo kutumikia wananchi kwa amani mpaka wakati wake ukifika.
Post a Comment