DUBE MIWILI TENA

Mshambuliaji wa Klabu ya Azam FC na mchezaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube amesaini mkataba wa miaka miwili kueendelea kuitumikia Klabu hiyo.

Mkataba huo utamfanya Dube kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2024.

Dube ambaye amesajiliwa msimu huu, amekuwa na kiwango bora kabisa hadi sasa akiwa ndiye kinara wa ufungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) akiwa na mabao 14.

Mbali na mabao hayo 14, kiujumla msimu huu, Dube amefunga mabao 17 kwenye mashindano yote, mengine matatu akitupia katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).
#BinagoSPORTS

No comments