MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Sylvester Mwakitalu, amefuta mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili masheikh waliokuwa mahabusu kwa tuhuma za ugaidi.
DPP amesema amewafutia mashtaka viongozi wote wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki) na kilichobaki ni utaratibu wa wao kutoka gerezani.
Hata hivyo, taarifa za kuaminika zilizolifikia dawati letu la habari asubuhi hii, zinasema Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem, tayari wameachiwa huru.
Awali, katika mwendelezo wa kesi yao namba 29 ya tangu mwaka 2014, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa mapendekezo kwa DPP ama kukamilisha haraka upelelezi au kuiondoa kesi ya watuhumiwa hao.
Hivi karibuni katika Baraza kuu la Eid, sehemu ya risala kuu iliyowasilishwa na Katibu wa BAKWATA, Nuhu Mruma, iliomba serikali kufikiria kuharakisha kutolewa kwa hukumu ya watuhumiwa hao.
0 Comments