• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / Habari / DANIEL CHONGOLO AKUTANA NA BI. WANG KE

    DANIEL CHONGOLO AKUTANA NA BI. WANG KE

    Bisaya Raphael June 01, 2021 Habari
    Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Ndg. Daniel Chongolo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke.

    Mazungumzo hayo yamefanyika Jana tarehe 31 Mei, 2021 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, ambapo Balozi huyo anayemaliza muda wake nchini Tanzania ametumia fursa hiyo kuwaaga wanaCCM na watanzania kwa ujumla, ambapo ameeleza kuwa, China na Mataifa mengine yanafurahishwa sana na mwenendo mzuri wa uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais na Mwenyekiti wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan na wanatarajia Tanzania kuendelea kupiga hatua zaidi za maendeleo.

    "Tunafuraha kuona kwamba, uongozi mpya ndani ya Chama na Serikali chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan unaendelea vema na uongozi umendelea kuwa imara na wenye tija kwa wananchi wake. Pia uongozi unaendelea kupata ushirikiano mkubwa sio tu ndani ya nchi bali na nje ya Tanzania. Hivyo tunaamini Tanzania itaendelea kupiga hatua zaidi za kimaendeleo." Balozi Wang Ke.

    Balozi huyo, kwa niaba ya serikali na watu wa China amemuhakikishia Katibu Mkuu kuwa, wataendelea kutoa ushirikiano wote kwa upande wa Serikali na Chama hasa kutokana na historia nzuri iliyopo kati ya CCM na Chama Cha Kikomunisti cha China CPC.

    Aidha, ametumia fursa hiyo kuipongeza CCM kwa kuvuka salama, kwa amani na utulivu mkubwa katika kipindi kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli, na kufanikiwa kumpata mwenyekiti mpya na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

    Wakati huo huo kwa upande wa Katibu Mkuu kwa niaba ya CCM ameitumia fursa hiyo kumuomba Balozi Wang Ke, kuendelea kuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini China kwa kuwa yeye amepata bahati ya kuishi hapa, na kujionea mwenyewe utulivu na amani iliyopo nchini.

    Pia, Katibu Mkuu amemuhakikishi Balozi kuwa, ushirikiano kati ya Tanzania na China, na kati ya CCM na CPC sio wa kutiliwa mashaka, ni uhusiano wa kindugu na umejengwa katika misingi ya kihistoria na kamwe hauwezi kutetereshwa.


    Related Posts

    Habari

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates