ADOLF MKENDA ATEMBELEA KAMPUNI YA SEED.CO
Katika kuendeleza ushirikiano na Sekta binafsi, ambalo ni jukumu la kisheria la Serikali kuhamasisha sekta binafsi katika uzalishaji wa Mbegu Bora, Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda katika ziara yake Jijini Arusha, Jana tarehe 30 Mei 2021 ametembelea moja ya kampuni binafsi ya uzalishaji wa Mbegu Bora za Kilimo nchini SEED.CO
Waziri Mkenda pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao wa Wizara ya Kilimo Ndg Nyasebwa Chimagu wamepata fursa ya kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo binafsi hasa katika suala zima la uchakataji na utunzaji wa Mbegu Bora unavyofanywa na kampuni hiyo kutoka hatua za awali Mbegu zinapotoka shambani, zinapopokelewa, kuchakatwa, kupimwa na kupakiwa tayari kwa kumfikia mkulima.
Katika ziara hiyo Waziri Mkenda amesema kuwa moja ya ajenda kuu ya Wizara ya Kilimo ni kuhakikisha nchi inazalisha mbegu za kutosha za kilimo kupitia sekta binafsi kadhalika Mamlaka ya Mbegu ya Serikali (ASA) ili kufikia hatua ya kujitosheleza katika uzalishaji mbegu na kuanza kuuza nje ya nchi.
Amesema kuwa serikali inahimiza Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) pamoja na Taasisi zote zinazojihusisha na utafiti hususani wa mbegu kuhakikisha kuwa zinazendelea kufanya utafiti wa mbegu bora na zitakazo ongeza tija katika kilimo.

Post a Comment