AMKA NA BWANA LEO 9

KESHA LA ASUBUHI

JUMATANO, JUNI, 9, 2021
SOMO: KUIPAMBA INJILI 

Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu. 

Ayubu 23:12. 



Ni wale tu wanaoisoma Biblia na kuona kuwa ni sauti ya Mungu inayozungumza nao ndio wanafunzi wa kweli. Hawa wanatetemeka mbele ya Neno la Mungu, kwani kwao ni uhalisia hai. Wanajifunza, wanatafuta hazina iliyofichika. Wanafungua ufahamu wao na moyo ili kupokea, na wanaomba neema ya mbinguni, ili waweze kufanya maandalizi kwa ajili ya wakati ujao, maisha yasiyo na kifo. 



Mwenge wa mbinguni unapowekwa mkononi mwake, mwanadamu anauona udhaifu wake, hali yake ya kutojiweza, akijiangalia haki yake mwenyewe. Ndani yake hakuna kitu ambacho kinaweza kumfanya afae mbele ya Mungu. Anamwomba Roho Mtakatifu, mwakilishi wa Kristo, ili awe kiongozi wake wa kudumu, akimwongoza katika kweli yote.... 



Kuukubali tu ukweli si dini ya Biblia .... Kuna Wakristo wengi ambao mioyo yao imefungwa katika ngao ya haki binafsi kiasi kwamba mshale wa Bwana, ulio wa kweli, unaorushwa kwa mikono ya malaika, unashindwa kupenya. Ukweli unawekwa pembeni, na roho haijeruhiwi. 



Mwanadamu anapaswa kumtafuta Mungu kwanza kwa ajili yake mwenyewe, kisha Roho Mtakatifu atauchukua ukweli wa thamani, ambao ni zaidi ya bei ya lulu, kama unavyotoka katika midomo ya Yesu, na kuupeleka kama nguvu iliyo hai katika moyo unaotii. Ukweli unaopokelewa moyoni unakuwa nguvu ya kuamsha akili, ikiamsha kila ufahamu. Ni ushawishi wa kiungu ambao unagusa moyo na kutengeneza muziki wa kimbingu unaotiririka kutoka kwenye midomo kwa shukrani halisi na sifa. 



Ah, sijui niseme nini ili kuamsha akili za wale ambao wanadai kuuamini ukweli, ili waweze kuipanda injili kwa imani inayofanya kazi kwa upendo na kuitakasa roho. Kristo anakuiteni mumtazame kama Mwasha nuru wa roho zenu zilizo gizani... 



Shauku ya wanadamu imewafanya kutafuta mti wa kujua mema; na mara nyingi wanadhani kwamba wanachuma tunda ambalo ni muhimu sana, kama Suleimani alivyotafiti, wanagundua kwamba ni ubatili mtupu kwa kulinganisha na sayansi ile ya utakatifu wa kweli ambao utawafungulia malango ya jiji la Mungu.... 



Kila mwanadamu anapaswa kuona kwamba kazi kubwa na muhimu kwa ajili yake katika maisha haya ni kupokea ufanana wa kiungu, kuandaa tabia kwa ajili ya maisha yajayo. Anapaswa kutumia ukweli wa kimbingu kwenye matumizi yake maalumu katika maisha halisi



—Manuscript 67, Juni 9, 1898,, “Chunguza Maandiko

No comments