ABDUL NONDO; SINA CHUKI NA MAKONDA
Sina chuki na Makonda @baba_keagan ila kama mwananchi nina mashaka tuu na utawala wake alipokuwa mtumishi wa umma ,kwamba fedha zetu za umma zilipigwa na kuna dalili zote kwamba fedha zetu za umma zilipigwa akiwa mkuu wa mkoa.
Sabaya alikamatwa sababu kulikuwa na allegations (Tuhuma /Malalamiko) mengi kutoka kwa watu dhidi yake ndio maana akasimamishwa,akachunguzwa na DPP kujiridhisha kwamba ana shutuma za kujibu hivyo kushtakiwa.
Mimi niulize kuna uzito upi kumkamata Makonda ili kuchunguza shutma(allegations) za ubadhilifu na mengine dhidi yake ?
@takukuru.tz Mnataka kusema hakuna viashiria vyovyote vinavyo wapa nguvu nyinyi ya kumchunguza Makonda ?
Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007 ,kifungu cha 27 kinasema " Ni kosa mtumishi wa umma kuwa na mali ambazo mwenye nazo hana maelezo ya kuridhisha kuhusu alivyozipata au kuwa na mali au pesa nyingi kuliko kipato chake halali " .
Kwangu mimi binafsi nina wasiwasi na fedha na mali za Makonda, alikuwa na nafasi ya Mkuu wa mkoa tuu.Ila hakuna aliyewahi jua wapi kwingine alikuwa anapata fedha kwa namna alivyokuwa anagawa na kutumia.
Tuhuma za matumizi mabaya ya mamlaka dhidi ya Makonda zilikuwa zinatolewa na watu wengi sana ,Je, takukuru kwanini hamtaki kujiridhisha kama ni kweli au sio kweli juu ya hizo tuhuma?
Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kusheku (Msukuma ) tar 7/Feb 2019 alitoa tuhuma Bungeni na kuandikwa kwenye Hansard dhidi ya Makonda,kwamba Makonda ana miliki mali nyingi tofauti na kipato chake akataja Gari Lexus ya Mil.400,magorofa Mwanza, ana miliki magari Toyota V 8 ,alikarabati ofisi yake kwa milion 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi (Chanzo Gazeti la mwananchi tar 8 Feb 2017,J.tano.).
Malalamiko mengine yalitolewa na aliyekuwa Mbunge wa Rombo ,Mh.Joseph Selasini Bungeni tar 11 , Februari 2017 na kuandikwa kwenye Hansard kwamba Makonda ana miliki jengo (Apartment) Viva Towers lenye thamani ya milion 600 alimzawadia Gari mke wake lenye thamani ya milion 550 kama zawadi ya Birthday (Chanzo Gazeti la Mwananchi February 11,2017).

Post a Comment