AMKA NA BWANA LEO 8
KESHA LA ASUBUHI
Jumanne 08/06/2021
*ENENDA UKAFANYE KAZI LEO*
*Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.* *Mithali 9:10*
*Kila roho imepewa uwezo. Hizi ni karama zinazopaswa kuboreshwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa uaminifu, ili kwamba Kristo atakapokuja aweze kupokea riba Yake*.
Tunasikia sana kuhusu elimu ya juu kama ambavyo dunia inalichukulia suala hilo. Lakini wale ambao hawajui elimu ya juu kama ambavyo ilifundishwa na kuoneshwa katika maisha ya Kristo, hawajui nini maana ya elimu ya juu. *Elimu ya juu maana yake ni kuishi kulingana na matakwa ya wokovu. Hukumbatia uzoefu wa kumwangalia Yesu kila siku, na kufanya kazi pamoja na Kristo kwa ajili ya kuwaokoa wanaopotea*.
*Kukaa bila kazi ni dhambi,* kwa maana kuna dunia ambayo inapaswa kufanyiwa kazi. Kristo aliyatoa maisha yake kwa ajili ya kazi ya kuwainua walioanguka na wenye dhambi. *Ingawa alikuwa Mfalme wa mbinguni, aliishi na kuteseka na kufa kwa kudharauliwa na kudhihakiwa na wanadamu wenye dhambi; ili kwa kufanya hivi aweze kuwaandalia jamii ya wanadamu makao huko mbinguni*. Kristo alitoa maelekezo ya utaratibu wa juu kabisa. Je, tunaweza kufikiria elimu ya juu kuliko ambayo tunaipata kwa kushirikiana na Yeye?
*Sasa ni wakati wetu wa kufanya kazi. Mwisho wa mambo yote umekaribia; usiku waja hivi karibuni ambapo hakuna mwanadamu ambaye anaweza kufanya kazi.* Usiku huu umekaribia sana kuliko ambavyo wengi wanadhani. Mwinue mtu wa Kalwari mbele ya wale ambao wanaishi katika dhambi. Kwa kalamu na sauti fanya kazi ya kufagia mawazo ya uongo ambayo yameteka akili za wanadamu kuhusu elimu ya juu.*
Kristo anampatia kila mtenda kazi amri, nenda ukafanye kazi leo kwenye shamba langu la mzabibu kwa utukufu wa jina Langu. Wasilisha mbele ya dunia iliyolemewa na upotovu baraka ya elimu ya juu ya kweli. *Nuru inapaswa kuangaza kutoka kwa kila muumini. *Waliochoka, waliolemewa, waliovunjwa moyo, waliotatizika,wanapaswa kuelekezwa kwa Kristo, chanzo cha uhai na nguvu za kiroho.*
*Tafuta elimu ya juu ambayo inafuata kikamilifu mapenzi ya Mungu, na kwa hakika utavuna zawadi ambayo inakuja kama matokeo ya kuipokea hiyo elimu. Utakapojiweka katika nafasi hiyo ambapo unaweza kuwa mpokeaji wa baraka za Mungu, jina la Mungu litatukuzwa kupitia maisha yako.*
*TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*
Post a Comment