MZINDAKAYA AFARIKI DUNIA
#TANZIA Mwanasiasa mkongwe nchini Dkt.ChrisantbMzindakaya amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Eligaesha amethibitisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, asikitishwa na kifo chake; @samia_suluhu_hassan
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa
za kifo Mzee wangu Dkt. Chrisant
Mzindakaya kilichotokea leo Jijini Dar es Salaam. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika uongozi wa nchiyetu, uzalendo na uchapakazi wake. Namuombea Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina."
Post a Comment