AMKA NA BWANA LEO 6
KESHA LA ASUBUHI
Jumapili 06/06/2021
*GHARAMA YA WOKOVU*
*Mwanangu, usiyadharau marudi ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.* *Waebrania 12:5, 6*
*Kristo ni mfano wetu. Alikaa katika mazingira magumu. Alistahimili mateso, alijinyenyekeza kwa ubinadamu*. Kristo alibeba mizigo yake bila kukata tamaa, bila kutindikiwa na imani, bila kulalamika. Aliyahisi majaribu Yake hata hivyo kwa sababu alikuwa Mwana wa Mungu. Huna shida, tatizo au ugumu ambao haukuwa na uzito sawa kwa Mwana wa Mungu; hakuna huzuni ambayo moyo wake haukuipata. Hisia zake ziliumizwa kwa urahisi kama za kwako. Lakini maisha na tabia ya Kristo haikuwa na doa. Tabia yake ilijumuisha ubora wa kimaadili, ikiwa ni pamoja kila kitu ambacho ni safi na cha kweli, cha kupendeza na chenye habari njema.
Mungu ametupatia mfano mkamilifu, usiokuwa na doa. *Mpango wa Mungu ni kukufanya uwe mtenda kazi mwenye uwezo na ufanisi. Akili aliyoifanya inapaswa kusafishwa, kuinuliwa na kuimarishwa.* Ikiwa akili itatumika katika kufanya mambo madogo, itakuwa dhaifu kama matokeo ya sheria zisizobadilika.
*Mungu anataka watumishi wake wapanue wigo wa mawazo na mipango yao ya kazi na kuleta uwezo wao ukutane na mambo ambayo ni makubwa, yanayoinua, na kuimarisha*. Hii italeta machipuo mapya katika akili. Mawazo yake yatachukua mawanda mapana na atafunga nguvu zake kwa ajili ya kazi yenye umuhimu mpana, wa kina na mkubwa, kuogelea katika maji mengi na yenye kina kirefu ambapo hakina kitako wala pwani.
*Mungu anaona mioyo na tabia za watu wakati wao hawaoni kwa usahihi hali zao. Anaona kwamba kazi na utume wake utaathirika ikiwa uovu hautasahihishwa ambao unakaa ndani yao bila kugundulika na hivyo kuachwa bila kusahihishwa. Kristo anatuita sisi watumishi Wake, ikiwa tunafanya anayotuamuru*.
*Kwa kila mwanadamu Mungu amempatia nafasi, sehemu na kazi, na Mungu haombi pungufu wala zaidi kuanzia wa chini kabisa, hadi mkubwa kabisa, kuliko wanavyopaswa kutimiza wito wao. Sisi si mali yetu wenyewe. Tumekuwa watumishi wa Kristo kwa neema. Sisi ni malimbuko ya damu ya Mwana wa Mungu.*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Post a Comment