AMKA NA BWANA LEO 3
*KESHA LA ASUBUHI*
ALHAMISI: JUNI 3 ,2021
SOMO: *MLANGO BADO UKO WAZI*
*Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;*
Mithali 2:6.
📌Katika ulimwengu kama wetu, ambapo ukweli na uongo unachanganywa kwa karibu kiasi kwamba ni vigumu sana kupambanua, ni jambo la hatari kupuuzia kutafuta hekima kutoka juu. Wale ambao sasa watazingatia na kurejea kwa Bwana bila kuchelewa, wakichukua nafasi yao katika msingi wa kweli, watapokea msamaha. Makosa yote yanachanganywa na ukweli, na hii inafanya udanganyifu wa Shetani uwe vigumu kuuona. Lakini wakati wa majaribu utakapotujia, itaonekana tofauti kati ya haki ya wenye haki na uovu wa waovu.
📌Kila kosa ni dhambi, na kila dhambi chanzo chake ni Shetani. Desturi potovu zimepofusha macho na kuhafifisha milango ya fahamu ya wanaume na wanawake. Sasa tunapaswa kujilinda katika kila hatua....
📌Wakazi wa ulimwengu, chini ya uongozi wa Shetani, wanafungwa katika matita tayari kwa ajili ya kuchomwa. Hatuna muda, wala dakika chache za kupoteza. Hukumu za Mungu zipo katika nchi, lakini wale ambao wataepuka, hawatashawishiwa na maonyo ambayo Mungu anayatuma, watafungwa katika vitita tayari kwa ajili ya kuchomwa. Hebu wachungaji na washiriki watoke waende katika shamba la mizabibu. Watayapata mavuno yao popote watakapoutangaza ukweli wa Biblia uliosahaulika. Wamishenari wanaume na wanawake, wanahitajika. Watawakuta wale ambao wanaukubali ukweli, na watachukua nafasi nyuma ya mwalimu wao ili kuzileta roho kwa Kristo....
📌Watu wengi wanapaswa kukusanywa katika kundi. Wengi ambao wameujua ukweli wameipotosha njia yao mbele za Mungu na wamejitenga na imani. Hadhi zilizovunjwa zitajazwa na wale waliomwakilisha Kristo kuwa anakuja katika saa ya kumi na moja. Kuna wengi ambao Roho wa Mungu anawasihi.
*✍️Muda wa hukumu ya Mungu ya uharibifu ni muda wa rehema kwa wale ambao hawana fursa ya kujifunza kujua ukweli ni upi. Bwana atawaangalia kwa upole. Moyo wake wa rehema umeguswa; mkono wake bado umenyooshwa ili kuokoa wakati mlango umefungwa kwa ajili ya wale ambao hawawezi kuingia. Idadi kubwa wataingia wale ambao wanausikia ukweli kwa mara ya kwanza katika siku hizi za mwisho*
—Barua ya 103, Juni 3, 1903,, kwa Mzee na Bi. George B. Starr, wafanyakazi wa uzeofu mkubwa kuhusiana na Ellen G. White nchini Marekeni na Australia.
*TAFAKARI NJEMA MPENDWA*
Post a Comment