AMKA NA BWANA LEO 24

KESHA LA ASUBUHI

ALHAMISI, JUNI, 24, 2021
SOMO: UONGOZI KATIKA MKANGANYIKO 

Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni;  mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto

Isaya 30: 21. 



[Edson] Unamhitaji Mshauri ambaye hatakosea; Yule ambaye uzushi hautaleta madhara; Yule ambaye fikra finyu hazitapotosha uwezo wake wa kufikiri. Njia inafunguka upande mmoja, lakini iwe ni njia kwa ajili yako kutembea kwayo au kuiepuka ni ile ambayo huitambui, na hakuna mwanadamu mwenye mwili wa kufa anayeweza kukueleza. 



Njia nyingine unafungwa mbele yako, na iwe ni kupita pembeni katika mwelekeo mwingine au kujali kusudi lako imara hakuna mwenye hekima wa kuweza kuelewa. Unamhitaji Kiongozi, nguvu isiyoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu, ambaye anaweza kujua nia yako na makusudi na ya moyo wako ili aongoze njia zako. Nyota ya Mashariki itaongoza njia zako, ikiwa tu utaifuata. 



Kamwe haupo peke yako. Haupo katika sehemu ambayo hakuna anayekujali. Baba yetu wa mbinguni amemtoa Mwana Wake afe kwa ajili yako. Msalaba wa Kalvari umeshuhudia kwamba anajali sana mambo yako, kwa sababu umenunuliwa na Mwana wa Mungu, na wewe ni mhusika wa maombi mengi. 



Ikiwa utajihisi sawa na kufanya kwa usahihi, yote yatakuwa sawa. Ikiwa utaomba msaada wa Mungu, hutaomba bure. Mungu yupo kazini kwa namna nyingi ili akuvute kwake. Hakuna kitu anachokifurahia sana zaidi ya kuona unaondolewa mzigo, njoo Kwake kwa ajili ya nuru na nguvu, na ameahidi kwamba utapata pumziko nafsini mwako. Ikiwa utapata moyo na sauti ya kuomba, atasikia, na ataushusha mkono wake ili akuokoe. Kuna Mungu ambaye anasikia maombi, na wakati ambapo nyenzo nyingine zozote zinaposhindikana, yeye ni kimbilio lako, kila msaada uliopo katika wakati wa mateso.... 



Ikiwa utakwenda kwa Mungu kwa moyo wa unyenyekevu wa imani ili kuomba uongozwe katika shida zako, basi ni fursa yako kumpatia shida yako. Mbingu na nchi zitapita kabla ahadi haijatimia. Kwa hiyo liamini neno la Mungu. Uliziamini ahadi zake ulipokuwa na miaka mitatu tu. Kuwa na usahili wa mtoto sasa, na njoo kwa Yesu ukiwa na imani ya kung’ang’ania. Mwamini Mungu kwa moyo wako wote, na ujasiri wako hautapuuzwa, wala hatakugeuzia mgongo. Mtazame Yakobo akimsihi Mungu katika mabonde ya Penueli. Ombi lake lilisikika na kujibiwa, na alipata ushindi 
mkubwa



—Barua ya 2, Juni 24, 1886,, kwa Edson na Emma White.

No comments