AMKA NA BWANA LEO 14

KESHA LA ASUBUHI

JUMATATU, JUNI, 14, 2021
SOMO: LINDA NAMNA ZA KUFIKIA WATU 

Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, aichukuapo miganda yake. 

Zaburi 126:5, 6. 



Mara nyingi tunakatishwa tamaa [James na Ellen White] katika matarajio yetu, lakini baadaye tunaona Bwana anavyofanya kazi katika jitihada zetu, na roho zinazomjia Kristo, ndipo tunaposahau uchovu, kukatishwa tamaa, na majaribu tunayokutana nayo kuhusiana na kazi hii na tunahisi tumeheshimiwa na Mungu kupata kibali cha kushiriki katika kazi. 



Tumekuwa na vipindi vizuri vya maombi pamoja na baadhi ya watu ambao walikuwa wamevunjika moyo na kukaribia kukata tamaa [katika mkutano wa makambi uliofanyika huko Iowa]. Tulifurahi pamoja nao pale nuru ilipong’aa katika vyumba vyenye giza vya roho. Kwa kweli Mungu amefariji mioyoni mwetu na ametuimarisha kwa ajili ya kazi yetu kubwa. Tunaamini kwamba matunda yatapatikana kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama matokeo ya mkutano huu. 



Hebu maombi yenu, watoto wangu [Edson na Emma], yapae mbinguni kwa niaba yetu, ili Mungu alete roho ambazo zipo katika giza la upotovu kuhusiana na maarifa ya ukweli.  Nuru, nuru ya thamani inang’ara katika kila ukurasa wa Neno la Mungu. Ndiye mshauri wetu. Tunapojifunza kurasa zake kwa shauku ya kutoka moyoni ili kuelewa wajibu wetu, malaika wapo karibu pembeni yetu ili kuifungua akili na kuimarisha fikra ili kufahamu mambo matakatifu yaliyofunuliwa katika Neno la Mungu. 



Kila wazo, neno na tendo, tunapaswa kulijaribu kwa ufunuo wa mapenzi ya Mungu. Katika mambo yote swali linapaswa kuwa, Je, hili litampendeza Mungu? Je, litakuwa sawasawa na mafundisho ya Neno Lake? Na wakati kunapokuwa na hali ya kutofanya maamuzi kwenye akili kuhusiana na wajibu, mioyo yetu ya asili itafuata hali ya kubweteka. Lakini, daima na tuiendee njia salama, haijalishi itahusisha kujikana nafsi kiasi gani. Hebu tukusudie kuingia katika hatari pale ambapo maslahi ya milele yanahusishwa. 



Kijana wangu mpendwa, Edson, yalinde kwa uaminifu mawazo yako. Kila nia ya moyo wako ilinde vizuri. Unapaswa kuweka vizuizi dhidi ya njia ya Shetani. Kuwa mwangalifu upande mmoja wakati upande mwingine umepuuzwa hakutafanikisha. Kuzembea upande mmoja kutasababisha matatizo kwa jeshi zima. Kuzembea kulinda njia moja kuelekea kwenye ngome kutasababisha mji kuanguka. Kuna taabu mbele yetu ambayo tunapaswa kukabiliana nayo, na usalama 
wetu pekee upo kwa Mungu.



—Barua ya 32, Juni 14, 1876,, kwa Edson na Emma White.



No comments