AHARIBU MAZAO BAADA YA MKE KUGOMA KUBAKI NYUMBANI

Mwanamume wa makamo katika kijiji cha Kamagambo huko Gichugu, kaunti ya Kirinyaga ameharibu mazao ya shamba yenye thamani inayokadiriwa kuwa na zaidi ya Ksh.200,000 baada ya mkewe kukataa kubaki nyumbani siku ya Wakina Baba Duniani.

Kulingana na mashuhuda, mtu huyo ambaye alitumia panga kukata ndizi za kijani kibichi na kukata magunia ya parachichi alisema kuwa mkewe alipaswa kukaa nyumbani kwa sababu ilikuwa Siku ya Baba.

Kulingana na majirani waliozungumza na Binago TV, mwanamke huyo anaishi kwa kuuza mazao ya shamba katika soko la Kitui siku za Jumapili.

Hellen Kaari Muriithi, mmoja wa wanawake ambao bidhaa zao ziliharibiwa, alisema kwamba waendesha boda boda walimjulisha kuwa kuna mtu ameharibu bidhaa zao.

Baada ya uchunguzi zaidi, waligundua kuwa mtuhumiwa huyo ameoa mmoja wa wanawake ambao ndizi zao zilikuwa zimeharibiwa.

"Mimi ni mmoja wa wale vitu vyao vimeharibiwa, tumefanya uchunguzi tukajua kwamba aliyeharibu ni bwana wa mama mmoja ambae huwa tunaenda nae sokoni kuuza," Hellen aliambia Binago TV

Hellen anakadiria kwamba alipoteza tatribani kiasi cha Ksh.15,000 katika shambulio la Jumapili juu ya ndizi kijani alichokuwa amekusudia kuuza.

Mfanyabiashara mwingine, David Muthike, ambaye maparachichi yake yalikuwa miongoni mwa mazao yaliyoharibiwa Jumapili asubuhi, alikadiria kuwa shambulio hilo liligharimu wafanyabiashara takribani Ksh. 200,000.

Kulingana na Muthike, mwanamume huyo, ambaye bado hajatambuliwa, alidai mkewe achukue siku hiyo kwa sababu ilikuwa Siku ya Baba.

"Mwanaume huyo alikuwa anasema bibi yake akae nyumbani ndio washerehekee siku ya Fathers Day," Muthike aliiambia Binago TV.

Tukio hilo la kushtua limewaacha wakaazi wakishtuka na wafanyabiashara hawajui hatua gani wachukue na iwapo kutakuwa na fidia.

No comments