Kufuatia uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kutengua Uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bw. Bakari Msulwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
Bi. Sheilla E. Lukuba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Ummy A. Mwalimu (Mb.) amemwelekeza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuteua Afisa atakayekaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo hadi nafasi ya Mkurugenzi itakapojazwa rasmi.
Aidha, Waziri Ummy amemwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Martin Shigella kuhakikisha anasimamia kwa karibu utendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikiwemo kuwapanga vizuri wafanyabiashara wadogo wadogo (Wamachinga) katika Manispaa hiyo bila kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji.
0 Comments