WAZEE SINGIDA WAMPOKEA BINILITH MAHENGE
Baraza la Wazee Mkoa wa Singida limempokea rasmi Mkuu mpya wa Mkoa, Dkt. Binilith Mahenge na kuahidi kumpa kila aina ya ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake.
Dkt. Mahenge ambaye kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliteuliwa na kuapishwa hivi karibuni kushika wadhifa huo kuchukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amestaafu.
Akizungumza na baraza hilo mkoani hapa, Dkt. Mahenge aliwaomba wazee hao kumpa ushirikiano ili kwa pamoja aweze kuongoza kwa ufanisi jahazi hilo lenye shabaha ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta mageuzi ya kiuchumi ndani ya mkoa.
"Singida ina kila kitu chema. Tuna Hali ya hewa nzuri inayokubali kila aina ya mazao...alizeti, ufuta, dengu, korosho na tunafuga sana, lakini zaidi tuna viwanda vya kutosha vya kukamua mafuta ya zao la alizeti," alisema Mkuu wa Mkoa.
Alihimiza kila mtu kwa nafasi yake likiwemo kundi la vijana, watendaji na wananchi wote kuwajibika kwa kuchapa kazi ili kupunguz

Post a Comment